Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu mwingine amvaa Rais Magufuli
Habari za Siasa

Askofu mwingine amvaa Rais Magufuli

Spread the love

MTU na atuhesabu hivi, kwamba sisi ni watumishi wa Kristo na mawakili wa siri za Mungu. Kumekuwa na tabia ya kushambulia watumishi wa Mungu pale walipozungumzia mambo ya kijamii.

Wakati mwingine mashambulizi yamevuka mipaka hata kuwachafua na kuweka vitisho. Kwa uzoefu wangu najua kwamba mengi ya yanayosemwa na watu hao ni ili kuvuruga ujumbe unaoletwa.

Mmoja wao akasema kwamba eti ananifahamu na amewahi kufanya kazi nami na kwamba nina kiburi. Kama nina kiburi basi ieleweke kwamba nina kiburi cha kumtumikia Mungu pasipo woga.

Mwingine akasema niliwahi kumsaliti Tundu Lisu kwenye kampeni ya madini. Hata Lisu mwenyewe anajua kwamba tulisimama pamoja kidete katika kupiga kelele kwa ajili ya uwekezaji mbovu kwenye sekta ya madini.

Hao wanaojifanya wanaona uchungu juu ya raslimali za nchi sikuwasikia wakati huo wakisema neno. Wengine wameshambulia viongozi wengine wa dini kwa ajili ya kulinda tu maslahi yao.

Mfano mzuri ni kumshambulia Baba Askofu Shao wa Zanzibar kwa ujumbe wake wa Krismasi. Kwa upande mwingine hatushangai kwa sababu ndivyo walivyofanyiwa manabii, mitume na mashahidi waaminifu wa Mungu katika historia.

Sote tunajua kwamba kuna wanafiki wengi ambao hawaitakii mema nchi yetu. Wazalendo wa kweli wa nchi wanasema ukweli juu ya jamii ili nchi ipone na si vinginevyo. Hatutakata tamaa maadam tu hatumuonei mtu na kamwe binafsi sitakuja kumuonea mtu hata siku moja.

Hata hivyo, niseme tu kwamba viongozi wa dini hawapigi kelele pale mambo yanapokwenda vibaya kwa sababu ya kujipendekeza. Kama yupo anayefanya hivyo basi ana tatizo kubwa.

Lakini pia hawafanyi hivyo kwa sababu wao ni malaika. Wanafanya hivyo kwa sababu wanao mzigo wa wito na utumishi wao. Kama yupo kiongozi wa dini anayezungumza kwa lengo la kuonea mtu, au kujipendekeza, au kupendeza watu fulani, basi huyo hamtumikii Mungu bali anajitumikia yeye binafsi na wale anaojipendekeza kwao.

Tusimuonee mtu na wala tusimpendelee mtu bali tuzungumze kama watumishi wa Mungu. Taji ya yale tusemayo iwe kweli na haki. Kristo amesema kwamba sisi tusiposema mawe yatazungumza.

Tena alisema kwamba ni afadhali tuingie mbinguni tukiwa na kiungo kimoja cha mwili (kwa sababu kiungo cha pili kitakuwa kimekatwa na wasiopenda kweli na haki), kuliko kwenda jehanam tukiwa na viungo vyote.

Tuwatendee watu wote kwa haki na kweli huku siku zote tukisema kweli na kusimama katika haki ili jamii ipone.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!