Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Kwa hili serikali kuweni wapole
Makala & Uchambuzi

Kwa hili serikali kuweni wapole

Spread the love

TAASISI za dini ni miongoni mwa wadau wakubwa wanaochangia kuwapo na kuendelea kustawisha amani ya nchi yetu ya Tanzania. Anaripoti Richard Makore … (endelea).

Lakini ni jambo la ajabu na kushangaza pale serikali inapozitisha kwamba itazifuta baadhi yao kwa madai kwamba zimeshindwa kuendana na masharti ya usajili wao.

Moja ya sababu zinazotolewa na serikali ni kwamba viongozi wa taasisi hizo za dini wanafanya mambo ambayo hayawahusu pale wanapotamka hadharani na kuwataka viongozi wa serikali watubu kwa Mungu.

Kutubu maana yake ni kupatana na aliyekupa uhai wa kuishi duniani sasa kwa hili sidhani kama ni kosa ambalo linaweza kuwafanya hawa viongozi wa dini waonekane wanafanya siasa katika nyumba za ibada.

Nyumba za ibada hazijawahi kuacha kufanya siasa na ndiyo maana kila viongozi wa dini wanapokutana na waumini wao wanafanya maombi ya kuwaombea viongozi mbalimbali wa serikali ili Mungu awaongoze vyema katika kuwaongoza Watanzania.

Kwa hili halijawahi kuitwa kosa wala kufanya siasa katika nyumba za ibada, lakini jambo la kushangaza ni pale viongozi mbalimbali wa dini wanawaotaka wanasiasa kutubu.

Viongozi wa kisiasa hawajawahi kukimbilia katika vyama vyao kwa ajili ya kuomba ama kuombewa bali hukimbilia kanisani kwa viongozi wa dini.

Hawa wanasiasa hukumbilia katika vyama vyao wanapotaka kufanikisha masuala yao ya kisiasa, lakini wanapohitaji baraka za Mungu wanakwenda kanisani ama msikitini.

Hivyo kwa namna yoyote ilivyo huwezi kutenganisha siasa na dini, lakini unaweza kufanya hivyo au inaonekana hivyo pale viongozi wa dini wanapokosoa wanasiasa.

Viongozi hawa wa dini hata wangetamka maneno mengi kiasi ilimradi tu yanasifia viongozi waliopo madarakani hapo hakuna kosa wala hapo hakuna siasa iliyoingia kanisani ama msikitini.

Hawa viongozi wa dini wanaongoza waumini wengi wakiwamo wanasiasa, kwa hiyo kuna haja ya kuachwa wawe huru ili watekeleze kazi zao za kuwaombea mema viongozi wa kisiasa na kuwakosoa pia wanapoona wanakwenda kinyume.

Kuingilia viongozi wa dini ni kutaka kuharibu amani iliyopo ambayo inahubiriwa katika nyumba za ibada na kila kiongozi wa dini.

Nilidhani baada ya viongozi wa dini kuwataka wanasiasa kutubu, kesho yake wangejaa katika nyumba za ibada na kufanya maombi siku nzima, lakini imekuwa kinyume na kilichotokea ni kwa serikali kuibuka na kuwatisha viongozi wa dini kwamba itafuta taasisi zao.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki amani yetu pamoja na viongozi wa kisiasa na wale wa dini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

error: Content is protected !!