Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nassari aanika ushahidi wa CCM kununua madiwani
Habari za SiasaTangulizi

Nassari aanika ushahidi wa CCM kununua madiwani

Spread the love

MBUNGE wa Chadema katika jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, ameanika ushahidi mwanana kuhusiana na mradi wa ununuzi wa madiwani, anaandika Saed Kubenea.

Mbele ya waandishi wa habari mjini Arusha, Nassari alimwaga ushahidi unaonyesha ushiriki wa kila mmoja katika mradi huo.

Akizungumza kwa kujiamini, Nassari alisema, kazi ya ununuzi wa madiwani inafanywa na viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi na kwamba ni mpango Maalum unaolenga kudhoofisha upinzani.

“Tunaweka ushahidi hapa ili huyu anayejiita mtetezi wa wanyonge na anayepiga vita rushwa anone na kuchukua hatua iwapo anachokinena ndicho anachotenda,” ameeleza.

Alisema, “kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakidang’anywa kuwa madiwani wetu wanaondoka ili kumuunga mkono Rais Magufuli. Kumbe siyo kweli.

“Leo tumekuja kuwadhihirishia kuwa wanaondoka kwa sababu wanashawishiwa na rushwa. Tumekuja hapa kuwapa ushahidi wa hilo.”

Nassari ambaye aliongozana na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alitoa kwa waandishi wa habari mkanda wa video unaomuonyesha mkuu wa wilaya ya Arumeru na mkurugenzi wa halmashauri wakishawishi madiwani kuondoka Chadema kwa ahadi za fedha na vyeo.

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja wiki mbili baada ya Rais Magufuli kupokea madiwani sita wa Chadema mkoani Arusha akidai kuwa kuondoka kwao kumetokana na kuvutiwa na sera zake.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Arusha, Rais Magufuli alisema kuwa kuondoka kwa madiwani hao “ni ushahidi mwingine wa kukubalika kwangu.”

Katika mkanda wa video wa Nassari, kunaonekana mkuu wa wilaya akimshawishi mmoja wa madiwani wa Arumeru kuondoka Chadema. Aliahidi kumlipia kiasi cha Sh. 10 milioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!