Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ndoto za Moshi kuwa jiji zayeyuka
Habari Mchanganyiko

Ndoto za Moshi kuwa jiji zayeyuka

Mji wa Moshi
Spread the love

AMRI ya Rais John Magufuli inayodaiwa kusimamisha mchakato mzima wa upanuzi wa mji wa Moshi kuwa Jiji ‘imewavuruga’ Madiwani wa Manispaa hiyo na sasa wamemwomba asikubali fedha za wananchi zilizotumika kwa zaidi ya miaka sita zipotee bure, anaandika Mwandishi Wetu.

Hatua hiyo inatajwa kuamsha hisia za wananchi walio wengi katika mji huo wa kitalii ambao tangu mwaka 2012 hadi Juni mwaka huu, ulikuwa ukitenga na kutumia hadi Sh. 40 milioni kila mwaka kwa ajili ya mchakato huo.

Waraka maalumu wa Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya unaeleza kuwa hivi sasa anafuata taratibu za kuomba kumuona Rais Magufuli ili awasilishe kwake taarifa ya mchakato mzima ulivyokuwa, kwa vile madiwani wanahisi kwamba alidanganywa.

“Hofu ya waheshimiwa madiwani kuhusu agizo la Rais imekuja wakati ambapo tayari Manispaa ilikuwa imeshasaini mkataba wa zaidi ya Sh. milioni 700 na kampuni za uaandaaji wa master plan (mpango kabambe) wa miaka 20 na walikuwa site (kwenye eneo la mradi).Sasa imesitishwa hadi tutakapopata GN (tangazo la serikali) kwa kuwa ile GN ya kilomita za mraba 58 ilifutwa na GN ya kilomita za mraba 142,” umeeleza waraka huo

Julai 15 mwaka 2016, Serikali ilitangaza mipaka mipya kwenye Gazeti la Serikali, Namba 219, Toleo la 29 ikionyesha eneo litakaloingizwa ndani ya mpango kabambe.

Hata hivyo, licha ya kutekelezwa kwa amri hiyo, Meya huyo amemuomba Rais Magufuli kupitia upya mchakato mzima wa upanuzi huo na \ikimpendeza airudishe GN ya kilomita za mraba 142.

Kwenye mipaka mipya, mpango huo ulikuwa umege kilomita za mraba 16 za Wilaya ya Hai na kilomita 68 za Jimbo la Moshi Vijijini.

Mtaalamu mshauri aliyekuwa akifanya kazi hiyo ya uandaaji wa mpango wa kabambe wa mwaka 2018/2038 ni Kampuni ya M/S CRM Land Consult (T) akizishirikisha kampuni nyingine za City Plan Consultant’s Ltd, Norplan (T) Ltd na Y& P (T) Architects Ltd, zote za Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Meya huyo: “Hoja za madiwani wa Moshi zinalenga kulinda kodi za wananchi zisipotee bure, kwa sababu kila mwaka Manispaa ilikuwa ikitenga kati ya Sh. milioni 25 hadi 40. Tulianza mchakato wa upanuzi si kwa kuamua wenyewe, bali tulihakikisha tunafuata taratibu zote za kisheria ili kuomba Jiji.”

Kwa sasa Tanzania inayo majiji manne pekee ambayo ni Jiji la Dar es Salaam linaloongoza kwa ukubwa, Mwanza, Arusha na Mbeya. Miji mingine iliyopo kwenye mchakato huo ni Dodoma na Moshi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!