Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Jiji la Dar es Salaam kinara wa matukio ya mauji
Habari Mchanganyiko

Jiji la Dar es Salaam kinara wa matukio ya mauji

Jiji la Dar es Salaam
Spread the love

JIJI la Dar es Salaam linaongoza kwa matukio ya mauaji yatokanayo na watu kujichukulia sheria mkononi yaliyofikia 117 katika kipindi cha nusu mwaka pamoja na ajali za barabarani, anaandika Mwandishi Wetu.

Nusu ya ajali zilizotokea nchini zimetokea Dar es Salaam na kwamba ajali zimekuwa ni sababu ya pili kwa vifo vya binadamu, ikitanguliwa na ugonjwa wa malaria.

Ripoti ya utafiti iliyotolewa jana jijijini na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuhusu haki za binadamu kwa kipindi cha miezi sita, Januari hadi Juni mwaka huu imebainisha hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo-Bisimba alisema haki ya kuishi ni kati ya hali zinazokiukwa ikiwamo watu kufia mikononi mwa vyombo vya dola, imani za kishirikina na ubakaji.

Pia alisema kuwa kati ya matukio 479 yaliyotokea katika kipindi hicho nchini, mauaji 117 yalitokana na wananchi waliojichukulia sheria mkononi, ikifuatiwa wa mikoa ya Mbeya (33), Mara (28) na Geita (26).

Alisema kati ya ajali 3,090 zilizosababisha vifo 1,308, vifo 126 vilitokea Dar es Salaam, ikifuatiwa na Mbeya (73), Tabora (61) na Arusha (69) likiwamo tukio la ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu na dereva wa shule ya St. Lucky Vincent.

Aidha, Bisimba alisema matukio ya ubakakaji yaliyotokea kipindi hicho yameongezeka Mara mbili, huku mkoa wa Iringa ukiwa kinara wa matukio ya kubaka.

Alisema kati ya 2,059 ya ubakaji yaliyoripotiwa Januari hadi Juni mwaka huu ni mengi ikilinganishwa na matukio 2,859 yaliyotokea mwaka mzima wa 2016.

“Iringa ubakaji upo juu, nusu mwaka watoto 121 wamebakwa, wamenajisiwa na kulawitiwa huku wengi wao wakifanyiwa na ndugu wa karibu kama, mjomba, kaka, baba mama babu,” alisema Bisimba.

Pia utafiti huo ulibaini mkoa wa Tabora unaongoza kwa matukio ya mauaji ya imani za kishirikina kwa kuwa na vifo 23 kati ya 115 yaliyoripotiwa vituo vya polisi nchini.

“Mauaji yanayohatarisha amani na usalama ni yale yaliyotokea maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji ambao watu 40 ikiwamo askari 13 waliuawa na watu wasiofahamika,” alisema.

Alibainisha kwamba licha ya Tanzania kutotekeleza adhabu ya hukumu ya kifo, katika kipindi cha miezi sita tayari watu saba wamehukumiwa adhabu hiyo na kwamba ni wakati kwa serikali kufuta adhabu hiyo ambayo haijatekelezwa tangu mwaka 1994.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!