Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Katibu wa Chadema afariki dunia
Habari za Siasa

Katibu wa Chadema afariki dunia

Spread the love

KATIBU mwenezi wa jimbo la Masasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Masasi mkoani Mtwara, Patrick Jacobo (48) amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia jana baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa pumu, anaandika Mwandishi Wetu.

Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Masasi, Leonard Undani amethibitisha kifo cha katibu huyo mwenezi na kusema Chadema ilipokea taarifa za kifo hicho leo saa kumi na mbili asubuhi.

Amesema walipokea taarifa hizo kwa masikitiko kwani katibu huyo alikuwa nguzo muhimu ndani ya Chama kutokana na jitihada zake katika kukipigania chama hicho katika mapambano ya kisiasa.

Undani amesema marehemu alianza kukitumikia chama mwaka 2012 akiwa kama katibu mwenezi wa chama hicho na katika mambo ya muhumu ambayo aliyafanya akiwa katika Chama ni pamoja na kuhamasisha watu kujiunga na Chadema ili kuendana na kasi ya vyama vingi.

“Kwa kweli kifo hiki kama chama ni pigo sana kwetu kwani alikuwa moja ya wapiganaji wa chama wazuri sana ndani ya chama chetu hatutamsahau kwa mchango wake katika Chama,” amesema Undani.

Amesema marehemu alikuwa ni mtu wa kujituma bila kuangalia masilahi yake bali alizingatia masilihi ya chama aidha alikuwa akijituma huku na kule kwa ajili kudumisha maendeleo ya chama.

Amesema Chadema wilaya ya Masasi imepata pigo kubwa kwa kupoteza mwanachama mwenye kila sifa ya kiutendaji katika chama na kwamba marehenu pia alikuwa na nafasi ya mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa wapiwapi Masasi hadi mauti yanamkuta hivyo Chadema wanatarajia kushiriki shughuli zote za mazishi kesho juma nne katika makabuli ya

Naye kaka wa marehemu, Abdu Bakari amesema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu kwa muda mrefu na jana alifariki ghafla saa kumi na moja alfajiri akiwa nyumba kwa mama yake mazazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape awaomba wadau wa habari wamuamini

Spread the loveWAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

error: Content is protected !!