Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi Dar wakamata watuhumiwa 200
Habari Mchanganyiko

Polisi Dar wakamata watuhumiwa 200

Baadhi ya vitu vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi
Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, limewakamata watuhumiwa mbalimbali wanaojihusisha na makosa mbalimbali ya kiuhalifu yakiwemo makosa ya kutumia madawa ya kulevya, anaandika Irene David.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya, amethibitisha hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Kanda Maalum ya Kipolisi ya Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya

Baadhi ya vitu vilivyopatikana ni pamoja na silaha moja aina ya ‘shot gun’ na risasi tano, televisheni ya ‘flat screen,’ zimu sana na aina mbalimbali za madawa ya kulevya.

“Mnamo tarehe 16 Julai mwaka 2017 majira ya saa tatu usiku maeneo ya Pemba Mnazi Kigamboni, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukamata silaha moja ikiwa na risasi ndani ya magazine, ” amesema Mkondya.

Aidha Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa wanne wakiwa kwenye bajaji yenye namba ya usajili MC 990 BLR rangi  ya bluu,wakiwa na televisheni ‘flat screen’ mbili za inchi 52 modeli ya LG, simu saba ambapo simu tatu ni aina ya Nokia, simu moja ni ya ‘sony ericson,’ simu moja ya ‘blackberry,’ ‘iphone’ moja, kamera moja aina ya sony, ‘hard disk’ tatu, kompyuta mpakato nne, chaja mbili za simu , ‘card reader’ moja na nyaraka mbalimbali.

Mkondya amesema, Jeshi la polisi linaendelea na kufanya msako mkali na mpaka sasa limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 200 kwa makosa mbalimbali yakiwemo makosa yanayohusiana na madawa ya kulevya, unyanganyi wa kutumia silaha, utapeli, wizi, kucheza kamari, kuuza pombe haramu na bhangi.

Mkondya amemaliza kwa kuwaasa Waanachi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuweza kutokomeza kabisa vitendo vya uhalifu nchini.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!