Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nape: Nitasema ukweli daima
Habari za SiasaTangulizi

Nape: Nitasema ukweli daima

Nape Mnauye, aliyekua Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Spread the love

ALIYEKUA Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Mnauye amesema ataendelea kusimamia ukweli daima kwa kila anachokiamini, anaandika Hamisi Mguta.

Nape ameyasema hayo leo akizungumza na wanahabari ikiwa ni siku moja baada ya uteuzi wake katika nafasi hiyo kutenguliwa na rais Magufuli.

“Nimefundishwa kusema kweli na kusimamia katika kila ninachikiamini, nimekua mzalendo kwa nchi yangu, nimekua muungwana kwa nchi yangu na naapa kuwa muungwana kwa nchi yangu, lakini mimi nimekua mzalendo kwa ccm ambayo nimeikuta kwenye shimo nikasimama kuiinua na watanzania wanajua. Kwa uzalendo huo ndiko nilipowaambia nitasema kweli daima,”amesema. 

Hatua ya kuondolewa kwa Nape katika nafasi hiyo ya uwaziri imekuja siku moja baada ya kupokea ripoti ya kamati ya uchunguzi aliyounda kwa tuhuma dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds Media akiwa na askari wenye zilaha za moto na kushinikiza watangazaji wa kipindi cha ‘The weekend chat show,’ (SHILAWADU) kurusha kipindi kwa maslahi yake binafsi.

Waziri Nape aliunda kamati ya uchunguzi kujua ukweli kwa kusikiliza kauli ya mwisho kutoka kwa mkuu wa mkoa baada ya kutembelea Clouds ili hatua zichukuliwe huku akiwa ameahidi kujing’atuka katika nafasi hiyo kama angeshindwa kusimamia tukio hilo kwakua ameingilia uhuru wa vyombo vya habari.

Chanzo:Rais Magufuli amkomoa Nape, kisa kamgusa Makonda

“Kwenye siasa usipopita kwenye migogoro bado haujakomaa, ili mbegu iote lazima ioze sasa mbegu niliyoipanda, mbegu ya kusimamia haki lazima iote,

“Kinachowakuitanisha watu sio magwanda ya kijani ni imani kwamba tuwe wakweli daima tuachane na fitna, nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko,”amesema.

Amesema, kuna watu wanataka kukaa mahali na kuwa waamuzi wa vijana wa kitanzania, hivyo ni lazima wakielewa kuwa hakuna la kuogopwa.

Nape ameeleza kuwa hana lakusema kwenye uwamuzi aliyoufanya rais lakini kwakua wakati anachukua uwamuzi wa kumchagua kulikuwepo na watu wengi ambao walikubali hivyo hawezi kukataa  na amejitahidi kutimiza wajibu wake.

“Wakati mimi nnateliwa sikuuliza kwahiyo wakati anataka kuweka Mtanzania mwingine sina sababu ya kuulizwa,”amesema.

Ameeleza kuwa kwakua hata Marehemu Julius Nyerere, Kawawa na wenzake kina mzee Mnauye walikuwepo wakaondoka, na viongozi waliopo sasa nao wataondoka, hivyo ni vyema kutafakari viongozi wanachukua uwamuzi gani kwa vizazi vya baadae na kuwa vitabaki na Tanzania ya namna gani.

“Kama alivyoniamini ndivyo anadhani kwamba nimetumika nimetosha anamuweka kaka yangu Harrison Mwakyembe namimi namuunga mkono  naamini atasimamia haki, nimefanya kazi kiwa mwaka mmoja na tasnia ya habari, tasnia ya sanaa, utamaduni na michezo, nawashukuru kwa dhati,” amesema.

Nape alifanya mkutano huo nje ya hoteli kutokana na tangazo kutoka kwa Meneja wa Hoteli hiyo kwamba walipokea ujumbe kutoka kwa RPC wa Wilaya ya Kinondoni, Suzan Kaganda kwamba wasiruhusu mkutano hivyo kuwatawanya waandishi kutoka nje huku maamuzi ya rais kumuondoa, kwenye uwaziri wakati ambao vyombo vya habari vikisubiri maamuzi ya mwisho kuhusu sakata hilo la kihistoria ambalo halijawahi kutokea limewacha midomo wazi kwakua Nape alikua mstari wa mbele kusimamia suala hilo.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!