May 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanasiasa, wadau wamtia moyo Nape

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama

Spread the love

WANANCHI na wadau mbalimbali wametoa maoni juu ya Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa Nape Nnauye aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, anaandika Pendo Omary.

Nape uteuzi wake umetenguliwa mapema leo na nafasi yake inachukuliwa na Harrison Mwakyembe aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria nafasi iliyojazwa na Prof. Palamagamba Kabudi.

Chama cha Wananchi- CUF kwa upande wake mapema leo baada ya kutolewa taarifa ya kuondolewa Nape kwenye nafasi ya uwaziri kimetoa tamko la kulaani hatua za Rais Magufuli katika uendeshaji wa nchi.

Sehemu ya tamko hilo lilolosainiwa na Julius Mtatiro, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF- Taifa inasomeka: “Mhe. Nape ameondolewa kwenye Baraza la Mawaziri kibabe na bila aibu kutokana na kusimamia Haki, Uhuru, Uwajibikaji, Nidhamu na Maadili ya uendeshaji wa vyombo vya habari nchini jambo ambalo ni jukumu la msingi la Wizara yake.”

Anthony Komu – Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema)

“Mh. Nape Nnauye ameitendea haki nafasi yake kwa vyovyote kuachwa kwake nje ya baraza la mawaziri, eti kwa kufuatilia alichofanya Makonda kutaanzisha ukurasa mpya ndani ya CCM. Sikio la kufa halisikii dawa. Namtakia Nape kheri tele; namwona akiwa huru na mwenye kheri zaidi.”

Hussein Bashe – Mbunge wa Nzega Vijijini (CCM)

You will never walk alone, I know you, we know you, Justice will prevail no matter how long it will take. Karibu back bench tutumikie Taifa letu, Majimbo yetu na Chama chetu usivunjike moyo. It’s just beginning of a New journey.

Richard Mabala – Mwanaharakati wa masuala ya maendeleo, haki za binadamu na jinsia.

“Heshima zako Ndugu Nape. Kwanza ulishirikiana na Ndugu Kinana kurudisha uhai wa chama kwenye ngazi ya jamii, ndiyo maana fulani aliweza kuchaguliwa. Na sasa umetetea heshima ya weledi wako pamoja na chama chako tena. Pole kwa yaliyokukuta na tuendelee kujenga Tanzania yenye misingi ya haki na demokrasia.”

Zitto Kabwe- Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo.

“Nape ni shujaa wa kizazi chetu.”

Mossy Magere – Mwandishi wa habari

“Hongera sana Nape, wewe ni shujaa wetu, ulishasema kupigania haki ni gharama lakini amini kisiasa umeinuliwa sana usisononeke jamii imekuamini. Tulilitegemea hilo lakini umeonesha msimamo na Wewe ni Shujaa uliyefia vitani.”

Vicensia Shule – Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

“Shujaa Nape Moses Nnauye, vitabu vya historia vitatakukumbuka. Kazi uliyotumwa na Watanzania umeitimiza kwa weledi na ujasiri mkuu. Bado utaendelea kuwa kiongozi mahiri, shupavu na mwenye misimamo dhahiri ya kutetea wanyonge. Karibu tuendeleze mapambano dhidi ya mifumo gandamizi, ya kinyonyaji na inayodhalilisha utu wa mwanadamu.”

Olivia Sanare – Kada ya CCM

“Nape Moses Nnauye Wewe Ni Mshindi. Haki imesimama na Taifa liko nyuma yako…..Uliyempa cheo leo ndio kakutumbua kwa kusimamia ukweli, tumeshajua ukweli hatufanyi makosa tena 2020 Mungu atupe Uzima.”

error: Content is protected !!