Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Azam FC yatwaa ubingwa bila nyavu zake kutikiswa
Michezo

Azam FC yatwaa ubingwa bila nyavu zake kutikiswa

Wachezaji wa Azam Fc wakishangilia ubingwa wa kombe la mapinduzi
Spread the love

BAADA Ya kuifunga klabu ya Simba na kuchukua ubingwa wa kombe la Mapinduzi kwa mara ya tatu, rekodi pekee iliyowekwa na klabu ya Azam Fc katika michuano hiyo ya mwaka huu ni kucheza jumla ya michezo mitano bila kufungwa wala kuruhusu goli lolote, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Goli pekee la Azam Fc katika fainali iliyopigwa jana lilifungwa na kiungo mkabaji Himid Mao kwa shiti la umbali wa mita 25, na kuipa klabu hiyo taji la tatu la michuano hiyo ya Mapinduzi inayofanyika kila mwaka visiwani Zanzibar.

Katika michuano hiyo Azam Fc ilicheza michezo yote bila kuruhusu goli hata moja, mchezo wa kwanza Azam Fc, ilicheza na timu ya  Zima moto na kuibuka na ushindi wa bao moja kwa bila na kwenda sare katika mchezo wa pili dhidi ya Jamhuri na baadae kuipa kipigo kikari Yanga cha mabao 4-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali na kupata ushindi wa bao moja mbele ya Taifa Jang’ombe na baadae kucheza fainali dhidi ya Simba.

Azam Fc ambayo katika michuano hiyo iliongozwa na kocha wake wa muda Iddi Cheche ambaye alikuwa akifundisha timu ya vijana, baada ya kutimua jopo la makocha kutoka nchini Hispania  kutokana na mwenendo mbaya wa timu katika michezo ya ligi kuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!