Monday , 5 June 2023
Home Kitengo Michezo Maamuzi ya CAF, Kuhusu rufaa ya TFF
Michezo

Maamuzi ya CAF, Kuhusu rufaa ya TFF

Langa Lesse Bercy mchezaji a timu ya Taifa ya Kongo chini ya miaka 17
Spread the love

BAADA ya sintofahamu ya muda mrefu juu ya rufaa ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) juu ya mchezaji wa timu ya taifa ya Jamuhuri ya Congo chini ya umri wa mika 17,Langa Lesse Bercy kutaka kujiridhisha kuhusu umri wake hatimaye kamati tendaji ya Shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF, limetoa nafasi ya mwisho kwa chama cha soka nchini Congo (FECOFOOT) kumpeleka kijana huyo Gabon kwa ajiri ya kipimo cha MRI, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Congo ilifuzu michuano hiyo baada ya kuitoa timu ta taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania, baada ya kuifunga bao moja kwa bila katika mchezo wa marudiano uliofabyika Kinshasa licha ya Tanzania kushinda katika mchezo wa kwanza kwa mabao 2-1 jijini Dar es Salaam.

Katika taarifa iliyotumwa na CAF katika shirikisho la soka nchini Congo, iliwataka kumpeleka mchezaji huyo ndani ya siku 10 kuanzia Januari 12, 2017 kwa ajiri ya kufanyiwa vipimo ili kujilidhisha juu ya umri wake kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.

Hii itakuwa mara ya tatu kwa CAF kumuita mchezaji huyo baada ya mara zote mbili kutokwenda kutokana na sababu mbali mbali wanazozijua shirikisho la mpira wa miguu nchini Congo.

Kwa mujibu wa kanuni za michuano ya kimataifa ya vijana wenye umri wa miaka 17, vijana wanaohitajika kucheza ni wale walio chini ya umri huo wa miaka 17.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Samia aipongeza klabu ya Yanga kwa hatua iliyofikia

Spread the love RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Yanga waitwa Ikulu kesho Jumatatu

Spread the love RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kesho Jumatatu, tarehe...

Michezo

Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa...

Michezo

‘EONII’ kuteka tasnia ya filamu

Spread the love  UZINDUZI wa Filamu ya Kisayansi ya ‘EONII’ uliofanyika Mei...

error: Content is protected !!