August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Timu Maalim’ wasusa mjengo wa ‘Timu Lipumba’

Wanachama wa CUF wakiwa nje ya Makao Makuu ya chama hicho, Buguruni, Dar es Salaam

Spread the love

SIKU, saa na dakika zinahesabika kwa Timu Maalim Seif Sharif Hamad kufungua ofisi mpya nje ya ile ya Buguruni jijini Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.

Wameamua kuachana na Ofisi Kuu ya chama hicho ambayo kwa sasa inatumiwa na Timu ya Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa, Timu Maalim wamefikia uamuzi huo baada ya Timu Lipumba kung’ang’ania kutumia ofisi ya Buguruni huku mgogoro uliopo ukiwa haujapatiwa ufumbuzi.

Ofisi mpya za CUF Timu Maalim zinatarajiwa kuzinduliwa muda wowote kuanzia sasa katika eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mbarara Maharagande, Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma amethibitisha kuwa, Timu Maalim inatarajia kuzindua ofisi hiyo muda wowote kuanzia sasa ili chama hicho kiendelee na operesheni zake kama kawaida.

error: Content is protected !!