Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Pareso, Mkuchika watunishiana misuli hela za TASAF
Habari za Siasa

Pareso, Mkuchika watunishiana misuli hela za TASAF

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalumu (Chadema), Cecilia Pareso ameitaka serikali kufanya tathimini na uchunguzi wa kina kuhusu matumizi ya fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kisha kuwasilisha bungeni taarifa ya matokeo ya uchunguzi huo. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Pareso ametoa ombi hilo leo tarehe 7 Septemba, 2018 wakati akiuliza swali  bungeni jijini Dodoma, ambapo amesema kuwa, fedha hizo hazijawahi kuonyesha matokeo ya moja kwa moja kwa wananchi waliopewa, huku akidai kwamba zimekuwa zikitumika kisiasa kama sehemu ya rushwa kwa ajili ya kushawishi wananchi kuichagua CCM ili ipate ushindi.

 “Swali la kwanza, fedha hizi za TASAF tunafahamu ni mkopo kutoka kwa World Bank (Benki ya Dunia), zimekuwa zikitolewa kwa kaya masikini na hazijawahi kuonyesha matokeo ya moja kwa moja kwa wananchi waliopewa, je serikali iko tayari kufanya uchunguzi wa kina na tathimini na kuleta taarifa hapa bungeni yenye kuonyesha matokeo ya moja kwa kaya hizi?” amehoji na kuongeza.

“Ni ukweli usiopingika kwamba fedha hizi za TASAF zimekuwa zikitolewa kisiasa kwa WanaCCM, na zinapofika chaguzi ndogo ili kushawishi kama sehemu ya rushwa kwa WanaCCMili ipate kuchaguliwa. Nini kauli ya serikali ikizingatia kwamba fedha hizi ni mkopo na zitarudishwa na watanznaia wote?”

Akijibu maswali hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Nkuchika amesema kuwa fedha za TASAF hazitumiki kisiasa ikiwemo kwenye chaguzi kutokana kwamba hakuna mtu mwenye ushahid juu ya madai hayo.

“Hela ya TASAF haitumiki katika uchaguzi. Fedha zinapelekwa na hazibaguliwi na kabla ya kutolewa kwa kaya masikini,  wananchi wa eneo husika hupendekeza kaya zinazostahili kupewa fedha hizo.

“Hakuna mtu anayechanganya siasa kweye TASAF, na wala hakuna ushahidi wa fedha za TASAF zinatumika kwenye uchaguzi, mimi ningeliweza kumuomba spika kwamba mheshimiwa athibitishe kauli yake lakini sitaki kufika huko nimemsamehe,” amesema.

Kuhusu taarifa ya matumizi ya fedha za TASAF, Waziri Nkuchika amejibu kuwa,  “Kwamba TASAF haijaonyesha matokeo, mimi naomba tusichanganye mambo, hoja ya kwamba mnaomba taarifa ya utekelezaji wa TASAF ikoje ni hoja ya msingi na inaweza aikaletwa.

“Mimi ndio waziri wa TASAFna juzi nilitoka Kilimanjaro na nimeona jinsi walengwa hasa kina mama walivyo jaribu kupambana na umasikini kwa kutumia fedha za TASAF.

“Namuomba muuliza swali, akubali ombi lake la kwanza kuomba taarifa ya TASAF, lakini kwa uhakika kamati husika ya bunge inapewa taarifa ya utekelezaji wa TASAF kila baada ya muda, mheshimiwa spika akisema taarifa ya TASAF inatak iletewe humu ndani italetwa.”

Aidha, Waziri Nkuchika ameahidi kufanyia kazi changamoto zinazoikabili mradi huo ikiwemo kuhakikisha kwamba serikali inaongeza fedha ili idadi ya kuongeza idadi ya kaya masikini zinazonufaika na fedha za TASAF.

Mradi wa TASAF ulianza rasmi mwaka 2013 na unatarajiwa kumalizika mwaka 2023 ambapo unatekelezwa katika kipindi cha miaka kumi mfululizo ambapo vimegawanyika kwa awamu mbili. Fedha za utekelezaji wa mradi huo ni za mkopo kutoka Benki ya Dunia (WB)

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Wazanzibar watarajia makubwa kutoka NMB Pesa Akaunti

Spread the loveWateja wapya wa Benki ya NMB wa Zanzibar wanatarajia neema...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kinana aungana na Tale kugawa mitungi ya gesi 800

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda amjibu Mwenyekiti UWT, “wananipa nguvu ya kuwapiga spana”

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukia Mwenyekiti wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madeni ya bilioni 219 yalipwa, wadai wengine waitwa

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia Mei mwaka 2021 hadi sasa imelipa madai...

error: Content is protected !!