Monday , 26 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wanajeshi 10 wahukumiwa kwa mauaji, ubakaji
Kimataifa

Wanajeshi 10 wahukumiwa kwa mauaji, ubakaji

Spread the love

MAHAKAMA ya kijeshi nchini Sudan Kusini imewahukumu wanajeshi 10 vifungo vya kati ya miaka saba na maisha kwa makosa ya mauaji na ubakaji. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Wanajeshi hao wamekutwa na hatia ya makosa hayo waliyoyatenda mwaka 2016 kwenye ghasia zilizotokana na shambulizi liliofanyika katika hoteli ya Terrain iliyoko mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba.

Katika ghasia hizo, mwandishi wa habari John Gatluak aliuawa, na wafanyakazi wa kutoa huduma za kibinadamu walibakwa.

Tukio hilo lilikuwa baya zaidi dhidi ya raia wa kigeni  tangu Wanajeshi wa Sudan Kusini kutuhumiwa kuendesha uhalifu mara kadhaa tangu yazuke mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!