Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa 1.5 Trilioni zipo wapi?
Habari za Siasa

1.5 Trilioni zipo wapi?

Spread the love

SI Bunge wala wananchi wanaojua kiasi cha Sh. 1.5 Trilioni ambazo hazikuonekana kwenye Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya 2016/17 zilipo. Anaripoti Yusuph Katimba…(endelea).  

Serikali kwenye Bunge hili la 14 itakuwa na kibarua cha kueleza umma matumizi ya fedha hizo ambapo ndani ya taarifa ya CAG 2016/17 haikueleza matumizi yake.

Mwanasiasa Zitto Kabwe, ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), ndiye aliyeibua suala hilo na kulivalia njuga wakati wa vikao vya Bunge la Bajeti.

Zitto, aliyedai kutumia ripoti ile ile ya CAG inayoishia Juni 30, mwaka juzi, alihoji ziliko Sh trilioni 1.5.

Hata hivyo, hoja ya Zitto ilijibiwa Aprili 20, mwaka jana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, aliyefafanua kuwa, katika fedha hizo kiasi cha Sh bilioni 697 kilitumika kwa matumizi ya dhamana na hati fungani zilizoiva na Sh bilioni 687 kilikuwa kwa ajili ya mapato tarajiwa.

Pia alisema kiasi cha Sh bilioni 203 kilikusanywa kama kodi kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Baada ya sakata hilo kuibuliwa tena bungeni Juni 5 mwaka jana na wabunge wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na John Mnyika (Kibamba) kulisababisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, kuwataka wabunge kutojadili kuhusu fedha hizo ndani ya Bunge hadi hapo PAC inayoifanyia kazi itakapowasilisha ripoti yake.

Kutokana na sakata hilo, Rais Dk. John Magufuli alimhoji CAG, Profesa Musa Assad na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, kuhusu ukweli wa madai ya upotevu wa fedha wakati alipowaapisha majaji wapya walioteuliwa Ikulu, Dar es Salaam na wote kwa pamoja walikanusha.

Mijadala ndani na nje ya Bunge n ahata ndani ya Ikulu haikuweza kutoa melezo yanaokinahisha zilipo fedha hizo. Miongoni mwa kazi kwenye Bunge hili la 14 ni kujadili ripoti hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!