Saturday , 13 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bungeni; Ni Serikali vs Wananchi  
Habari za SiasaTangulizi

Bungeni; Ni Serikali vs Wananchi  

Spread the love

MKUTANO wa 14 wa Bunge la Jamhuri unaanza leo tarehe 29 Januari 2019 ambapo pamoja na shughuli zingine, hatma ya maoni ya wananchi na mapendekezo ya serikali katika Muswada wa Sheria wa Vyama vya Siasa yatajulikana kabla ya kuhitimishwa kwa bunge hili. Anaandika Yusuph Katimba…(endelea).

Kwa wiki kadhaa kumekuwepo na mikutano iliyoendeshwa na Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria katika kupata maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya muswada huo.

Taasisi mbalimbali zikiwemo za dini, siasa, wanaharakati na kada zingine tayari zimewasilisha mapendekezo yao kuhusu muswada huo. Wananchi hao wameainisha maeneo kadhaa ambayo wangependa yafanyiwe kazi kwa maslahi ya taifa na demokrasia nchini. Miongoni mwa maeneo hayo ni:-

Pendekezo la msajili kupewa mamlaka ya kupata taarifa yoyote kutoka ndani ya chama cha siasa kwa maana kuwa, anaweza kuomba utaratibu wowote wa chama katika kujiendesha jambo ambalo wananchi wameona halina afya hasa katika uwanda wa siasa za ushindani.

Wananchi wanaamini kuwa, kwenye mazingira haya msajili ambaye ameteuliwa na mwenyekiti wa chama cha siasa, anaweza kuomba taarifa inayoweza kutumiwa na chama tawala kwa maslahi ya chama hicho hivyo wametaka kifungu hicho kiangaliwe upya.

Wananchi wameonesha kutoridhika na Kifungu cha 4 ambacho kinampa mamlaka msajili kufuatilia michakato ya chaguzi na teuzi za ndani ya chama na kuridhia ama la.

Wananchi wana hofu kwamba, msajili anaweza kuamua kinyume na matakwa ya chaguzi za chama kwa kutowatambua ama kutoridhia waliochaguliwa na vikao halali vya chama kwa utashi wake binafsi. Wameshauri suala hilo libaki ndani ya chama husika.

Kifungu 5B ni miongoni mwa vifungu vinavyoonekana kuwa na kasoro. Kwenye kifungu hicho msajili amepewa mamlaka ya kuomba taarifa yoyote kutoka kwenye chama.

Wananchi wanasema ‘hapana’ kwamba msajili ambaye ni mteule wa mwenyekiti wa chama tawala, anaweza kukusanya taarifa zinazohitajika maslahi ya chama tawala na kuwa, msajili adhibitiwe kwamba sio kila taarifa anayoitaka kwenye chama lazima apewe.

Kifungu 18 kimempa mamlaka msajili kusitisha ruzuku kwa utashi wake. Wananchi kwenye maoni yao wameonesha kuamini kuwa, iwapo msajili atapewa mamlaka hayo ni wazi kuwa, anaweza kufanya hivyo kwa chama kinachoonekana kuwa mshindani wa chama tawala kwa ajili ya kukidhoofisha.

Kifungu kipya cha 21E kinampa mamlaka msajili kusimamisha uanachama wa mwanachama wa chama cha siasa. Wananchi wanaamini kuwa ni kazi inayopaswa na chama cha siasa chenyewe kwa maslahi ya chama cheke.

Wananchi waliopata kutoa maoni yao, hawajaridhishwa na muswada kukataza vikundi vya uhamasishaji kukatazwa kwa kuwa, ili chama kiweze kukua kinahitaji uwepo wa vikundi vinavyohamasisha wananchi kujiunga na vyama hivyo.

Lakini pia wananchi wameshauri mtego uliopo kwenye muswada huo wa kutaka vyama kuungana ndani ya siku 21 kabla ya kupendekezwa kwa wagombea wa uchagaguzi mkuu uondolewe kwa kuwa, unanyima fursa vyama vya siasa kufanya chaguzi za ndani za wagombea na kisha kwenda kujinadi.

Pia taasisi na makundi mbalimbali yameonesha kutoridhika na faini pia vifungo vikubwa vilivyoweka kwenye muswada huo na kuomba kuwa, faini hizo zinaonekana kukomoa badala ya kutoa mwelekeo chanya.

Bunge litakuwa na kazi ya kuunganisha maoni ya wananchi na mapendekezo ya serikali ili kuunda sheria inayoweza kukubalika na wadau wote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za Siasa

Chadema yapuliza kipyenga uchaguzi viongozi kanda

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza maandalizi ya uchaguzi...

Habari za Siasa

CCM :Hatutaki ushindi wa makandokando uchaguzi Serikali za mitaa

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakihitaji ushindi wa makandokando katika...

Habari za Siasa

Makala: Puuzeni wanasiasa wanaojigamba wanaweza kubadili maamuzi ya mahakama

Spread the loveKATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

error: Content is protected !!