Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mtolea aonja jeuri ya upinzani bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Mtolea aonja jeuri ya upinzani bungeni

Abdallah Mtolea, aliyekuwa Mbunge wa Temeke
Spread the love

ABDALLAH Mtolea, Mbunge wa Temeke ameapishwa leo tarehe 29 Januari 2019 bungeni mbele ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wa CUF Kambi ya Prof. Ibrahim Lipumba pekee. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mtolea ameapishwa leo baada ya kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika mwishoni mwa Disemba mwaka jana kwenye jimbo hilo. Mbunge huyo awali aliiwakilisha CUF kwenye lakini tarehe 15 Novemba mwaka jana alijiuzulu.

Wakati akiingia bungeni kuapishwa, wapinzani hawakuwemo, walisubiri baada ya kuapishwa kwake ndio wakaingia bungeni wakionesha kutomuunga mkono kwa hatua yake ya kujiunga na ‘mpinzani’ wao.

Tofauti na ilivyo kawaida ya wabunge waliojiunga na CCM wakitokea upinzani, mbwembwe zilizozoeleka za kuwasindikiza waliojunga nao zilikuwa hafifu. Mtolea aliyevalia suti ya bluu alisindikizwa na chereko chache na kisha kuapishwa na Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri.

Baada ya kuapishwa Mtolea alikwenda kumsalimia Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!