Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya WHO yataharuki, maambukizo yafika 105,000 kwa siku
Afya

WHO yataharuki, maambukizo yafika 105,000 kwa siku

Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO
Spread the love

WAKATI Serikali ya Tanzania ikinadi kupungua kwa maambukizo mapya ya virusi vya corona, Shirika la Afya Duniani (WHO), limeeleza dunia kufikia rekodi ya maambukizi ya kiwango cha juu kwa siku. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Kwa saa 24 zilizopita, WHO limerekodi maambukizo mapya 106,000, kiasi ambacho hakijawahi kufikiwa ndani ya saa 24 tangu maambukizi hayo ya zuke mwishoni mwa mwaka 2019.

WHO imeeleza kuwepo kwa maambukizo ya kasi katika nchi zilizo na kipato cha chini na cha kati na kueleza kwamba ‘ni jambo linalosikitisha.’

Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO ameonesha wasiwasi wake kuhusu ongezeko hilo ambapo mpaka sasa, zaidi ya watu 330,000 duniani kote wameripotiwa kufariki.

“Katika kipindi cha saa 24 zilizopita, kumekuwa na maambukizo mapya 106,000 ambayo yameripotiwa kwa WHO ambayo ni makubwa zaidi kuandikishwa kwa siku moja toka janga la corona lianze,” Dk. Tedros ametoa kauli hiyo jana jioni Jumatano tarehe 20 Mei 2020 na kuongeza:

“Karibia theluthi mbili ya walioathirika, wameripotiwa katika nchi nne pekee,” ametoa onyo kwamba, safari ya kupambana na janga corona bado ni ndefu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!