July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanawake washika kasi Urais Z’bar, wagombea wafika 26

Fatma Kombo Masound

Spread the love

MBIO za kuwania Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 zinazidi kushika kasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya mwanamke wa tatu kujitoka kwenye harakati hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Tangu shughuli ya uchukuaji na urejeshaji fomu ilipoanza tarehe 15 hadi 30 Juni 2020 imeshuhudia viongozi waliopo madarakani kama mawaziri, wakuu wa mikoa na watoto wa Marais wastaafu wa Zanzibar wakijitosa kwenye mbio hizo.

Leo Jumatano tarehe 24 Juni 2020, Fatma Kombo Masound amekuwa mwanamke wa tatu kuchukua fomu kuwania kumrithi Rais Ali Momahed Shein, ambaye anamaliza muda wake wa uongozi wa miaka 10.

Hasna Atai Masoud

Wanawake wengine waliojitosa kwenye kinyang’anyiro hicho  ambacho wagombea wamefikia 26 ni; Hasna Atai Masound aliyechukua fomu mapema leo Jumatano asubuhi na Mwatum Mussa Sultan.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Fatma aliwaeleza waandishi wa habari kwamba hana la kuzungumza na apewe fursa ya kwenda kuzisoma fomu hizo kujua anapaswa kufanya nini.

Mwantum Mussa Sultan akiwa na fomu za kuwania Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Wengine 25 waliokwisha kuchukua fumo ni;

 1. Mbwana Bakari Juma
 2. Ali Abeid Karume
 3. Mbwana Yahya Mwinyi :
 4. Omar Sheha Mussa
 5. Hussein Ali Mwinyi
 6. Shamsi Vuai Nahodha
 7. Mohammed Jaffar Jumanne
 8. Mohammed Hijja Mohammed
 9. Issa Suleiman Nassor
 10. Makame Mnyaa Mabarawa
 11. Mwatum Mussa Sultan
 12. Haji Rashid Pandu
 13. Abdulhalim Mohammed Ali
 14. Jecha Salum Jecha
 15. Dk Khalid Salum Mohammed
 16. Rashid Ali Juma
 17. Khamis Mussa Omar
 18. Mmanga Mjengo Mjawiri
 19. Hamad Yussuf Masauni
 20. Mohammed Aboud Mohammed
 21. Bakari  Rashid Bakari
 22. Hussein Ibrahim Makungu
 23. Ayoub Mohammed Mahmoud
 24. Hashim Salum Hashim
 25. Hasna Atai Masound
error: Content is protected !!