Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi Mkuu 2020: Mbatia amtumia salamu bosi wa NEC
Habari za Siasa

Uchaguzi Mkuu 2020: Mbatia amtumia salamu bosi wa NEC

James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi
Spread the love

CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kimetuma ujumbe wa Jaji Semistocles Kaijage,  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuhakikisha watendaji wake wanatenda haki kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatano tarehe 24 Juni 2020 na James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, wakati anazungumzia na waandishi jijini Dar es Salaam kuhusu mustakabali wa chama chake, kuelekea uchaguzi huo.

Mbatia amemueleza Jaji Kaijage kwamba, anapofanya maamuzi yake kuhusu uchaguzi huo, akumbuke kwamba amebeba mustakabali wa maisha ya Watanzania, katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mwenyekiti huyo wa NCCR-Mageuzi amesema, ili NEC iheshimike kwa wananchi, inatakiwa itekeleze majukumu yake, pasina kupata shinikizo lolote la kisiasa.

“Ili NEC iheshimike, rai yangu kwa  Jaji Kaijage, watumie heshima ya ujaji kufanya maauzi sahihi kwa kuwa uchaguzi ni tukio linaelezea ni maisha gani ya Watanzania yatakuwa kwa miaka mingine mitano ijayo,” amesema Mbatia.

“Hatma ya Watanzania iko mikononi mwa Jaji Kaijage na makamishina wa tume, waangalie sheria ya uchaguzi na wale wasaidizi bila kupata shinikizo lolote la kisiasa ili haki itende kwa wote na ionekane kutendeka.”

Aidha, Mbatia amewataka wadau wa uchaguzi kueleza changamoto zinazojitokeza mapema ili zitatuliwe, badala ya kulalamika baada ya uchaguzi kufanyika.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage

“Wenye dhamana ya NEC, kama kuna mtu unamtilia mashaka usisubiri katikati ya mchezo ndio uanze kulalamika, tuwaondoe sasa kwa maandishi ukweli ni huo,” amesema Mbatia

Mbunge huyo wa Vunjo amesema, “unakuta mkurugenzi wa uchaguzi unamuona ni mpendeleaje yuko kwenye vyama vingine, hawezi kusimamia uchaguzi na haki isipokuwepo inakuwa ni shida.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!