Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Upinzani wapata pigo DRC
Habari za SiasaKimataifa

Upinzani wapata pigo DRC

Etienne Tshisekedi kiongozi wa chama cha upinzani cha (UDPS)
Spread the love

KIFO cha Etienne Tshisekedi kiongozi wa chama cha upinzani cha (UDPS) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kimeacha simanzi na pigo kwa wapenda mageuzi nchini humo, anaandika Wolfram Mwalongo.

Tshisekedi aliyekuwa na umri wa miaka 84 amefariki dunia akiwa mjini Brussels, Ubelgiji alipokuwa akipatiwa matibabu ingawa hadi sasa tarifa za ugonjwa uliokuwa ukimsumbua hazijawekwa wazi.

Taarifa hizo zimenyong’onyeza wapinzani nchini Kongo huku baadhi wakiamini kwamba kuondokewa na kiongozi huyo ni pigo kubwa katika mapambano ya kutetea demokrasia katika taifa hilo lenye historia ya vita za wenyewe kwa wenyewe.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba, enzi za uhai wake Tshisekedi alikuwa mstari wa mbele kupinga waziwazi ukiukwaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia na ufisadi.

Mbali na kuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Rais king’ang’anizi madarakani, Joseph Kabila lakini pia kiongozi huyo aliwahi kushika nafasi mbalimbali wakati wa utawala wa Mobutu Sese Seko kabla ya kujiuzulu waliposhindwa kuafikiana katika maamuzi aliyodai yanakandamiza wananchi.

Taarifa zaidi kutoka nchini Kongo zinadai kuwa kiongozi huyo alikuwa akitarajiwa kushika nafasi ya juu ya uongozi katika serikali ya muungano ambayo ingeundwa baina ya wapinzani na Rais Kabila hadi pale uchaguzi mkuu utakapofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!