Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa kitendo cha Mwalimu kumpiga mwanafunzi hadi kufa ni cha bahati mbaya. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).
Ndalichako amesema Serikali haijamtuma Mwalimu huyo kufanya tukio hilo hivyo watu wasichukulie tukio hilo kudhani kuwa shule ni sehemu ambayo si salama.
Amesema ikiwa siku moja baada ya kifo cha Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kibeta mkoani Kagera kutokea huku ikidaiwa kuwa kilitokana na kipigo cha Mwalimu aliyemtuhumu kwa kumuibia pochi yake lake.
Aidha amewataka Watanzania wawe na amani na utulivu katika kipindi hiki ambacho serikali inafanya kazi yake.
“Aliyefanya hivyo hajatumwa na serikali, nawaambia shule ni sehemu salama kwa namna yoyote asitokee mtu akawafanya wazazi wahofie kuwapeleka shule watoto wao,”amesema.
Leave a comment