WAGOMBEA wa urais wawili wenye nguvu nchini Kenya, Raila Odinga (NASA) na Uhuru Kenyatta (Jubilee), leo wamepiga kura katika uchaguzi mkuu nchini humo huku kila mmoja akisisitiza suala la kulinda amani, anaandika Mwandishi Wetu.
Kenyatta amepiga kura katika eneo lao la asili alipozaliwa la Gatundu na Odinga alikwenda na kupiga kura katika eneo la Kibera.
Misululu ya wananchi wa Kenya imeonekana leo nchini humo, lakini wananchi katika maeneo mbalimbali wakionekana watulivu na wanaofuata utaratibu.
Inaelezwa kuwa kuna baadhi ya maeneo yanakabiliwa na mvua na kusababisha usafiri kuwa mgumu katika sehemu hizo.
Hata hivyo imeripotiwa kuwa katika maeneo ya Embakasi kulikuwa na ucheleweshaji wa kuanza kupiga kura.
Wapigakura milioni 20 nchini humo wanatarajia kupiga kura katika uchaguzi huo ambao unaonekana kuwashindanisha vigogo hao wawili Odinga na Kenyatta.