Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea kuchangia 20mil ujenzi wa zahanati
Habari za Siasa

Kubenea kuchangia 20mil ujenzi wa zahanati

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa Kimara
Spread the love

SAED Kubenea, Mbunge wa Ubungo (Chadema), ameahidi kutoa Sh. 20 milioni, kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya mitaa ya Kilungule A na B, iliyopo kata ya Kimara, Jimbo la Ubungo, Jijini Dar es Salaam, anaandika Irene Emmanuel.

Kubenea, alitoa ahadi ya fedha hizo, leo wakati wa hafla ya kukabidhi hati za umiliki ardhi na majengo kwa wakazi wa Kimara iliyofanyika katika eneo la kanisani, Kilungule.

Akiongea mbele ya Waziri wa Nyumba, Ardhi na Makazi, William Lukuvi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo, Meya wa Manispaa ya Ubungo na Diwani wa kata ya Kimara, Kubenea amesema: “… nimeiomba manispaa ya ubungo inunue eneo lilopo hapa Kilungule kwa ajili ya ujenzi wa zahanati. Mimi ninaweka milioni 20 za kuanzia ujenzi, ninaomba jambo hili lifanyike haraka.”

Kubenea amesema, “nitashirikiana na Diwani na uongozi wa Serikali za mitaa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kuhakikisha zahanati hiyo inajengwa na kukamilika ndani ya kipindi cha miaka miwili ijayo. Hii ni kwa sababu matatizo ya afya katika eneo la Kilungule ni makubwa na kwamba wagonjwa wanalazimika kwenda kimara Baruti na au Mavurunza ambako ni mbali kwa wakazi hawa.”

Mbunge huyo wa ubungo, amemuunga mkono na kumpongeza Waziri Lukuvi kwa kufanya maendeleo kwa wananchi bila kujali itikadi ya vyama vyao.

Katika hatua nyingine, Kubenea ameahidi kuchonga barabara, yenye urefu wa kilomita 1.9 itokayo Kimara Baruti msikitini, kuelekea Kilungule kwa lengo la kupunguza usumbufu kwa wananchi wanaotumia barabara hii.

Barabara ya Kimara baruti Kilungule, imeharibika vibaya na haipitiki kirahisi na vyombo vya moto jambo ambalo katika baadhi ya maeneo abiria wanashushwa kwenye magari au bajaji ili waweze kupita katika hayo maeneo korofi.

“Ninafahamu matatizo ya barabara yenu, nimekaguqa barabara hiyo, na nimejionea mwenyewe jinsi barabara ilivyo haribika. Hivyo basi, nimeamua kuchukua posho yangu ya ubunge ili kukarabati barabara hiyo kwa lengo la kuwasaidia wananchi wangu muondokane na adha vya usafiri,” alieleza Kubenea huku wananchi wakimshangilia.

Hafla ya kukabidhi hati-urasmishaji wa ardhi na makazi-umeratibiwa na benki ya dunia kupitia wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!