August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema kuchambua sekta ya elimu nchini

Susan Lyimo, Waziri Kivuli wa Elimu

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinatarajia kuandaa mkutano na waandishi wa habari ili kuchambua hali ya sasa ya elimu ya juu nchini, anaandika Hellen Sisya.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho leo hii, Halima Mdee, mbunge wa Kawe, amesema kuwa chama chake kupitia kwa Suzan Lyimo, Waziri Kivuli wa Elimu, kitatoa hali halisi ya elimu ya juu ilivyo kwa sasa.

“Serikali inatumia visingizio kubagua Watanzania, na sisi hili suala hili tutalikemea, tutaendelea kulikemea na tutaanda mkutano kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa kina wa elimu.

Hata hivyo, Mdee amesema siku na tarehe ya kufanya mkutano huo haijapangwa na kwamba dhamira ya kufanya uchambuzi huo wanayo kama chama.

error: Content is protected !!