Sunday , 25 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Majeshi ya nchi 7 kuonyesha umahiri Tanga
Kimataifa

Majeshi ya nchi 7 kuonyesha umahiri Tanga

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi
Spread the love

MAJESHI ya nchi saba za Jumuiya ya Maendeleo  ya  Afrika (SADC), yameanza mazoezi ya kijeshi yenye lengo la kujiandaa na tishio la mashambulizi ya kigaidi na uharamia yanayoitikisa dunia, anaandika Mwandishi wetu.

Akizungumza katika uzinduzi wa mazoezi hayo yanayozishirikisha nchi saba zilizopo kwenye jumuiya hiyo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, wanajeshi wa nchi hizo watabadilishana uzoefu wa namna ya kukabiliana na vitendo vya kigaidi na uharamia.

Dk Mwinyi ameeleza kuwa mazoezi hayo  yatawawezesha askari kupanua uzoefu katika masuala ya ulinzi na  kuimarisha  Umoja wa Maendeleo wa Nchi za Kusini (SADC).

“Tuna lengo la kujiweka tayari kwa misaada ya kijeshi katika kupambana na ugaidi na uharamia, baada ya hapo watapata uzoezfu mkubwa katika kukabiliana na vitendo hivyo vya kiharamia” amesema.

Ameeleza faida zitakazopatikana kutokana na mazoezi hayo  kufanyika Tanga na nchini kwa ujumla  ni pamoja na wananchi kupata tiba  kipindi chote cha mwezi mzima pamoja na ujenzi wa miundombinu.

Kwa upande wake,  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance  Mabeyo  amesema zaidi  ya askari 600  kutoka nchi za Botswana, Lesotho, Zimbabwe, Afrika Kusini, Zambia, Malawi na Tanzania  watashiriki katika mazoezi hayo yatakayodumu kwa mwezi mzima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

Kimataifa

Jeshi Kongo lazima jaribio la M23

Spread the loveJeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Jumatano lilizima...

KimataifaTangulizi

Rais wa Namibia amefariki dunia

Spread the loveHAGE Gengob, Rais wa Namibia, amefariki dunia wakati akipokea matibabu...

error: Content is protected !!