SAFARI ya mwisho hapa duniani ya aliyekuwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza inahitimishwa leo Ijumaa tarehe 26 Juni 2020. Anaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea)
Mwili wa Nkurunziza aliyefariki dunia ghafla tarehe 8 Juni 2020 kwa shinikizo la damu unazikwa leo Ijumaa Mji wa Gitega katikati ya Burundi.
Nkurunziza alifikwa na mauti, ikiwa imesalia miezi miwili kukabidhi madaraka kwa Rais mteule wa wakati huo, Jenerali Evariste Ndayishimiye.
Kutokana na kifo hicho, Jenerali Ndayishimiye aliapishwa tarehe 18 Juni 2020 na leo anaongoza maelefu ya Warundi, wageni mbalimbali wa ndani nan je katika shughuli hiyo ya mwisho kwa mwili wa Nkurunziza.
Hadi anafikwa na mauti, Nkurunzinza alikuwa ameongoza Taifa hilo kwa miaka 15 kuanzia 2005-2020.
Nkurunziza hadi anafikwa na mauti alikuwa na miaka 55. Alizaliwa tarehe 18 Desemba 1964.
Kabla ya maziko, shughuli imeanza asubuhi katika uwanja wa mpira wa Ingoma mjini Gitega kisha mwili wake kupitishwa mbele ya wananchi watakaokuwa uwanjani humo kumwaga na baadae kufanyika maziko rasmi.
Baadhi ya wageni waliohudhuria ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete na mkewe, Salima.
Leave a comment