Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Milioni 780 kupambana na dawa za kulevya Tanga 
Afya

Milioni 780 kupambana na dawa za kulevya Tanga 

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imepata Sh. 780 milioni  kwa ajili ya kujenga kliniki ya huduma za methadone kwa waathirika wa dawa za kulevya mkoani Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea).

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa kituo cha muda cha kutoa tiba ya methadone kwa warahibu wa madawa ya kulevya kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga – Bombo.

“Kwa kushirikiana na wadau wetu wa maendeleo Mfuko wa Dunia (Global Fund) na Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya tumepata zaidi ya milioni 780 na tumezileta kwa ajili ya kujenga jengo la kutolea huduma ya methadone” amesema Waziri Ummy.

Hata hivyo, Waziri Ummy ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Tanga kwa ubunifu walioufanya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo PEPFAR na Amref -Tanzania, kwa kujenga kituo cha muda kwa ajili ya kutoa tiba kwa warahibu wa madawa ya kulevya ambacho kimegharibu shilingi milioni 20 za Kitanzania.

“Tumeona tunaweza kufanya huduma hizi kwa gharama nafuu, nnafurahi kuona kwamba zimetumika takribani shilingi milioni 20 kwa ajili ya kutengeneza kituo cha muda kwa huduma za kliniki katika Mkoa wa Tanga” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema, ilikuwepo haja ya kuwa na kliniki ya methadone kwa Mkoa wa Tanga kutokana na kuwa na waathirika wengi wanaotumia madawa ya kulevya huku mkoa huo ukishika nafasi ya pili ya kuwa na warahibu wengi wa madawa ya kulevya.

“Mkoa wa Tanga unashika nafasi ya pili ya kuwa na idadi kubwa ya watumiaji wa dawa za kulevya, takwimu za mwaka 2016 zinaonyesha Tanga una watumiaji taribani 5190 wa madawa ya kulevya” amefafanua Waziri Ummy.

Amesema hadi sasa kuna kiliniki nane ambazo zinatoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam kliniki hizo zimeanzia katika hospitali ngazi ya mikoa na kushuka chini kwenye hospitali za ngazi ya halmashauri .

Ametaja maeneo yatakayofuata kuwa na huduma hizo ni pamoja na Bagamoyo, Kigamboni, Mbagala, Tegeta pamoja na Magereza Segerea.

Amesema kwa mujibu wa Takwimu za Wizara ya Afya, Tanzania ina waathirika 8,071 waoapatiwa huduma ya dawa za methadone kwa ajili ya kupunguza madhara ya dwa za kulevya ambapo kati yao wagonjwa 480 ni wanawake na 7591 ni wanaume.

Naye Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, James Kaji amesema wiki hii Tanzania inaungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya kupinga madawa ya kulevya ambayo kwa mwaka huu kauli mbinu ni tujenge uelewa sahihi kwa tatizo la dawa za kulevya ili kuimarisha mapambano dhidi ya tatizo hilo.

“Uzinduzi wa kituo hiki ni muendelezo wa vituo vingine nane vinavyotoa huduma nchini ambapo kwa Dar es Salaam vipo vitatu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na Temeke; Mbeya – Hospitali ya Rufaa ya Nyanda za Juu Kusini; Mwanza – Hospitlai ya Rufaa ya Sekou Toure; Bagamoyo na Dodoma – Itega” amefafanua Kamishna Jenerali James Kaji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela amesema, Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya shughuli za usafirishaji wa madawa ya kulevya na kufanya kuwa na idadi kubwa ya watumiaji ambao hiingia kwenye urahibu wa dawa hizo..

Aidha Shigela ameiasa jamii kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya huku akiwaomba kutoa taarifa kwa mamlaka kwa wale wanaojihusisha na usafirishaji na biashara ya madawa ya kulevya.

“Kwa wale ambao wameathirika na madawa ya kulevya katika jamii zetu tuwaone ni kama sehemu ya ndugu zetu, tusiwanyanyapae, tuwaelekeze na tuwalete kwenye matibabu na tunaamini watarudi kwenye hali ya kawaida,” amesisitiza Shigela.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!