November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kushambuliwa Lissu, Mbowe: Chadema ‘tumepoteza imani’

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakina imani na uchunguzi unaofanywa na Jeshi la Polisi kuhusu viongozi wake walioshambuliwa. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 25 Juni 2020 na John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo ya Mnyika imekuja siku chache baada ya Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) kusema, jeshi lake halijamalizana na Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema aliyeshambuliwa tarehe 7 Septemba 2017.

“Hatuna imani na uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi, kama tulivyotangaza kwa tukio la Lissu, chama kinaendelea kutafakari hatua za ziada za kuchukua.

“…lakini kwa sasa tungependa wananchi wapuuze hizi njama za jeshi kutumika kuhalalisha kauli za uongo zilizotolewa kisiasa,” amesema Mnyika.

Akizungumzia kauli ya IGP Sirro kuhusu Lissu kukwamisha uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwake, Mnyika amepinga sababu hiyo akisema, Jeshi la Polisi ni wajibu wake kuchunguza tukio, hata kama mhanga hayupo.

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema

“…katika hali ya kawaida, nikiri hadharani Jeshi la Polisi limeshindwa kuchunguza tukio, au IGP atoe majibu kwa umma kwa nini mpaka sasa hawajakamilisha uchunguzi huo,” amesema Mnyika.

Lissu na Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama hicho katika wakati tofauti, walishambuliwa na watu wasiojulikana, wakiwa kwenye makazi yao jijini Dodoma.

Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 2020, wakati Mbowe alishambuliwa usiku wa kuamkia tarehe 9 Juni 2020. Hadi sasa, Jeshi la Polisi halijaeleza kukamatwa kwa wahusika.

Akieleza kushambuliwa kwa Mbowe, Mnyika amesema Chadema ina mashaka na kauli iliyotolewa na IGP Sirro, kwamba mwenyekiti huyo alitoa taarifa za uongo kuhusu kushambuliwa kwake.

error: Content is protected !!