May 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Milioni 18 wapona corona dunia

Spread the love
MAAMBUKIZO ya virusi vya corona (COVID-19) duniani yamefikia milioni 26.18, waliopona milioni 18.44 na waliofariki kutokana na ugonjwa huo ni 867,370. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea)

Mtandao wa worldometer unaonyesha leo Alhamisi tarehe 3 Septemba 2020 Marekani inaongoza kwa kuwa na maambukizo milioni 6.29, waliopona milioni 3.54 na waliofariki 189,964.

Brazil inashika nafasi ya pili kwa kuwa na maambukizo milioni 4, waliofariki dunia 123,899 na waliopona milioni 3.2.

China ambako corona ilianzia mwishoni mwa mwaka 2019, inashika nafasi ya 38 ikiwa na maambukizo 85.077 na waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo ni 4,634 na waliopona ni 80,251.

error: Content is protected !!