Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Chadema asikitishwa na majibu ya mawazili
Habari za Siasa

Mbunge Chadema asikitishwa na majibu ya mawazili

Naibu Waziri wa Fedha, Dk. Ashantu Kijaji
Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Suzana Mgonukulima (Chadema) amesema anasikitishwa na serikali kutoweza kujibu maswali kwa ufasaha na badala yake wanajibu kisiasa. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo aliitoa leo bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kutaka kujua kama serikali ina mpango wa kukwamisha halmashauri ambazo zinaongozwa na upinzani au la kutokana na kutozipatia fedha za maendeleo halmashauri hizo.

Katika swali lake la nyongeza amesema kuwa kwa sasa mapato yanayotokana na makusanyo katika halmashauri yanapekekwa serikali kuu lakini hakuna fedha zinazorudi katika halmashauri kwa ajili ya maendeleo licha ya kuwa halmashauri imekuwa ikiomba fedha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua ni kwanini isitungwe sheria ya kuibana serikali ikiwa haitarejesha fedha za kodi kwenye halmashauri, kwenye miji, Manispaa na Majiji.

“Lengo la Serikali ni kuingiza fedha zote za kodi kwenye mfuko moja kwa moja na baadaye asilimia Fulani ya fedha hizo zirudishwe kwenye halmashauri.

“ Je ni kwanini isitungwe sheria ya kuibana serikali ikiwa haitarejesha fedha za kodi kwenye halmashauri, kwenye miji,Manispaa na Majiji,” alihoji mbunge huyo.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Fedha, Dk. Ashantu Kijaji amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya bajeti ya mwaka 2015 kifungu namba 58 usimamizi wa mapato utazingatia misingi mbalimbali.

Aliitaja misingi hiyo kuwa ni mapato yote ya serikali kuingizwa kwenye mfuko mkuu wa serikali, yoyote aliyepewa mamlaka ya kukusanya mapato ya serikali atawajibika ipasavyo katika ukusanyaji wenye ufanisi, utunzaji wa hesabu, utoaji wa taarifa na kuzuia ufujaji wa mapato.

Aina nyingine aliyoitaja Dk. Kijaji ni mapato yote kuingizwa kwenye sheria ya kuithinisha matumizi ya fedha za serikali.

Aidha alisema kuwa kwa mujibu wa kifugungu cha 44 cha sheria ya bajeti, mgawo wa fedha utazingatia bajeti iliyoithinishwa, upatikanaji wa mtiririko wa fedha, utekelezaji mpango wa manunuzi na mpango wa kuajiri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!