Sunday , 25 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyabiashara Moro wapigwa marufuku kupanga biashara ardhini
Habari Mchanganyiko

Wafanyabiashara Moro wapigwa marufuku kupanga biashara ardhini

Spread the love

WAFANYABIASHARA ndogondogo wanaopanga biashara zao chini katika maeneo mbalimbali Mkoa wa Morogoro wamepewa siku 14 kuhakikisha wanaweka bidhaa zao kwenye meza ili kuepuka magonjwa kwao na kwa wateja wao. Anaripoti Christina Haule … (endelea).

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Steven Kebwe amesema hayo jana wakati akizindua usajili na utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi (Machinga) kwenye Hafla ya kubabidhi vitambulisho vya kufanya biashara hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao makuu.

Dk. Kebwe amesema, kupanga biashara chini kwa ajili ya kuuza kwa wanunuzi kwa mahitaji ya nyumbani si salama ambapo kunaweza kusababisha bidhaa kuingia uchafu ikiwemo vinyesi na hivyo kumfanya mteja kupata magonjwa ya tumbo.

Hivyo amewataka wafanyabiashara hao kuzingatia siku hizo 14 walizopewa ambapo licha ya kuepuka magonjwa pia wataufanya mji kuwa katika muonekano wa hali ya usafi.

Aidha amesema kuwa atakayekiuka agizo hilo atachkuliwa hatua ikiwemo kuondolewa kwenye sehemu anayofanyia biashara.

Hata hivyo ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kufuata agizo la Rais Magufuli la kuacha kuwaondoa wafanyabiashara hao kwa kuwakimbiza huku wamewashikia virungu bali wafuate sheria na taratibu zilizowekwa.

Pia Dk. Kebwe aliwataka wafanyabiashara kuzitumia vyema fursa za biashara zilizopo mkoani hapa ikiwemo mazao ya mpunga kuzalisha na kusindika wenyewe kwa ajili ya kupata faida wenyewe na kuweza kulipa kodi tofauti na ilivyo kwa sasa bidhaa hiyo kuchukuliwa na wafanyabiashara wa mikoani na kubandika majina yao wenyewe.

Naye Kamishana wa kodi za Ndani Elija Mwandumya amesema, tayari vikundi 1851 vikiwa na wanachama 17,601 kutoka katika maeneo mbalimbali mkoani hapa vimeshatambuliwa ambapo vikundi 473 vilipewa mafunzo na vikundi 143 vyenye wanachama 2,324 vimeshasajiliwa.

Amesema kuwa kati ya wanachama hao 2,324 ambao vikundi vyao vimesajiliwa wanachama ambao ni wafanyabaishara 361 kutoka kwenye ni vikundi hivyo wamekabidhiwa vitambulisho vyao jana.

Mwandumbya amesema kuwa lengo la TRA ni kuhakikisha wanatambua wafanyabiashara ndogo nchini na Serikali inapanga mipango mizuri ya kuwafanya waendeleze vizuri biashara zao na kuhakikisha wanafikia uwezo wa kulipa kodi.

Naye Mfanyabiashara wa wafanyabishara wadogo Manispaa ya Morogoro, Faustine France ameuomba uongozi wa Manispaa ya Morogoro kuona umuhimu wa kuzungumza na uongozi wa wafanyabiashara hao ili kuweza kuweka utaratibu mzuri wa meza kwa wafanyabaishara hao.

France amesema, uwezekano wa kila mfanyabiashara kuwa na meza yake ni mdogo lakini pia haitaleta picha nzuri katika Manispaa ambapo ni vema wafanyabiashara wakawa na meza za kuchangia ili kuweza kufanya biashara zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari Mchanganyiko

“Jamii ielimishwe faida za uhifadhi”

Spread the loveWIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ili kukabiliana na migongano...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza Nathwani alivyomshambulia jirani yake

Spread the loveSHAHIDI ambaye ni fundi Seremala, Dominic Mpakani (43) ameileza mahakama...

Habari Mchanganyiko

DCEA, TAKUKURU waunganisha nguvu kupamba na dawa za kulevya, rushwa

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!