MBUNGE wa Siha Dk. Godwin Mollel (Chadema) ameihoji serikali na kutaka ieleze ni kwa nini hospitali zake nyingi zinakosa dawa muhimu za binadamu wakati katika hospitali binafsi zipo, anaandika Dany Tibason.
Mollel aliuliza swali la nyongeza amesema kumekuwepo na tatizo la hospitali nyingi na vituo vya afya vya serikali kukosa dawa muhimu za binadamu huku dawa hizo zikipatikana katika vituo binafsi au maduka binafsi .
Awali katika swali la msingi la mbunge wa Korogwe mjini, Mery Chatanda( CCM) alitaka kujua serikali imetoa maelekezo gani pale ambapo Bohari ya Dawa (MSD) wamekuwa hawana baadhi ya dawa zinazohitajika kwa wagonjwa.
“Hospitali za serikali zimeandaliwa kupata huduma za MSD lakini wakati mwingine baadhi ya dawa hazipatikani na hospitali hairuhusiwi kununua dawa nje ya MSD.
“Je serikaki imetoa maelezo gani pale ambapo MSD wamekuwa hawana baadhi ya dawa hizo zinazohitajika na wagonjwa”alisema.
Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk.Khamis Kigwangwala alisema kuwa kwa sasa hospitali zote pamoja na vituo vya afya vya serikali kuna dawa zaidi ya aina 138 zinazohitajika.
Alisema kuwa kwa sasa dawa nyingi zinapatikana kutokana na kuongezeka kwa pesa katika wizara husika tofauti na ilivyo kuwa hapo hawali.
Leave a comment