Monday , 26 February 2024
Home Habari Mchanganyiko JWTZ yaunda kikosi maalum kusaka silaha
Habari Mchanganyiko

JWTZ yaunda kikosi maalum kusaka silaha

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi
Spread the love

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Husein Mwinyi ameliambia Bunge kuwa kwa sasa kimeundwa kikosi kazi kwa ajili ya kusaka silaha za kivita ambazo zinatumiwa na watu wenye nia mbaya, anaandika Dany Tibason.

Dk.Mwinyi ametoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Chambani,Yusufu Salim Husein(CUF).

Katika swali la nyongeza mbunge huyo alitaka kujua serikali inachukua hatua gani ili kuweza kuthibiti kuzagaa kwa siraha za kivita ambazo zinaonekana kutumika vibaya kwa kuwajeruhi watu mbalimbali.

“Tunajua kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ndilo lenye jukumu la mipaka ya nchi ya kimataifa, sina shaka na usalama wa Mipakana,lakini ndani ya nchi hakuko salama je kuna utaratibu gani ambao unatumika kwa kuzagaa kwa silaha za kivita ambazo zinatumiwa kuwadhuru watu”alihoji Hussein.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Mkoani, Twahir Awesu Mohamed(CUF) alitaka kujua serikali imejipanga vipi kuimarisha amani hapa nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Tembo aongoza migongano binadamu, wanyamapori

Spread the loveIMEELEZWA kuwa asilimia 80 ya migongano baina ya binadamu na...

Habari Mchanganyiko

“Watanzania tembeleeni vivutio vya utalii”

Spread the loveSHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka Watanzania kujitokeza kutembelea...

error: Content is protected !!