BARAZA la Mitihani la Taifa Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Necta Zanzibar, Dk. Charles Msonde amesema ufaulu kwa mwaka huo umeongezeka kutoka 97.58% hadi kufikia 98.32% mwaka 2019 ikiwa ni sawa 0.74%.
Amesema kuwa mtihani watahiniwa 91,298 walisajiliwa wakiwamo wasichana 37,948 ambao ni sawa na 41.56% na wavulana 53,350 sawa na 58.44% ambapo kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 80,216 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa ni 11, 082.
“Kati ya watahiniwa 91,298 waliosajiliwa kufanya mtihani , watahiniwa 90,001 sawa na asilimia 98.58 walifanya mtihani na watahiniwa 1,297 sawa na asilimia 1.42 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ugonjwa na utoro, watahiniwa wa shule, kati ya watahiniwa 80,216 waliosajiliwa, watahiniwa 79,770 sawa na asilimia 99,44 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa 33,883 sawa na asilimia 99.57 na wavulana 45,887 sawa asilimia 99.35. Watahiniwa 446 sawa na asilimia 0.56 hawakufanya mtihani,” amesema.
Leave a comment