Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Afya Bilioni 7 kujenga jengo la wazazi Mbeya
Afya

Bilioni 7 kujenga jengo la wazazi Mbeya

Spread the love

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya inajenga jengo la Wazazi lenye thamani ya Sh. 7 bilioni ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na Nyanda za Juu Kusini. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Ummy Waziri, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameyasem hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na ujenzi wa miradi katika Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya.

Amesema kuwa Serikali imedhamiria kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya nchini ikiwemo huduma za kibingwa ili kuondoa usumbufu kwa Wananchi wanaohitaji huduma hizo kwa kusafiri umbali mrefu jambo linalopelekea gharama kubwa na usumbufu kwa wananchi.

“Tunajenga jengo la wazazi na watoto wachanga la ghorofa sita, ambalo litakuwa na jumla ya vitanda 200, vyumba vitatu  vya upasuaji kwa ajili ya wanawake wajawazito ,vyumba sita kwa ajili ya uangalizi maalum (ICU) kwa wanawake wajawazito, pia vyumba  maalum vinne kwa ajili ya vitoto vichanga (NICU),” amesema. 

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amemwagiza Mkandarasi wa majengo hayo kuhakikisha wanaharakisha ujenzi wa majengo hayo ili wananchi waanze kupata huduma mapema jambo litalosaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto  nchini.

Aidha, Waziri Ummy ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nyanda za juu kusini kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili kurahisisha gharama za matibabu.

“Nitoe Wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nyanda za juu kusini ili waweze kufurahia huduma nzuri lazima wajiunge na huduma za Bima ya Afya, Kuna NHIF Toto Afya kadi kwa mtu yoyote mwenye umri wa chini ya miaka 18 ni Sh. 50,400 huduma mwaka mzima ndani ya Mbeya na Tanzania kwa ujumla,” amesema.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa katika kila wanawake 100, wanawake 85 wanajifungua bila matatizo yoyote, huku akisisitiza kukamilika kwa ujenzi huu kutasaidia kukokoa wanawake 15 waliobaki kutokana na huduma Bora zakibingwa zitakuwa zikitolewa.

Dk. Godlove Mbwanji, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kukubali kutenga fedha ili kujenga jengo la ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200 jambo litalosaidia kutatua changamoto ya ufinyu wa nafasi.

“Tunapenda kutoa shukurani za dhati kwa Serikali ya awamu ya tano, kwa kukubali kutenga fedha kupitia Wizara unayoiongoza ili kuweza kujenga jengo la ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta, ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200.” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Waziri wa Tamisemi apewa siku 14 afike Morogoro kutatua changamoto za Afya

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel...

Afya

Ma-RMO, DMO watakiwa kujitafakari ubadhirifu hospitali za mikoa, wilaya

Spread the love  NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, amewataka waganga...

Afya

JK atoa ya moyoni kuhusu huduma za afya

Spread the love  RAIS Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete amesema huduma za afya...

AfyaHabari za Siasa

Heche amvaa Ummy Mwalimu kisa bima ya afya

Spread the love  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche amemtaka...

error: Content is protected !!