Monday , 5 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli ‘amweka ndani’ mtoza ushuru kwa dakika 5 
Habari za Siasa

Rais Magufuli ‘amweka ndani’ mtoza ushuru kwa dakika 5 

Rais John Magufuli alipokuwa ziarani mkoani Kagera
Spread the love

MTOZA ushuru aliyetambulika kwa jina moja la Pesha, jana tarehe 11 Julai 2019, alijikuta matatani baada ya Rais John Magufuli kuagiza akamatwe na kuwekwa ndani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tukio hilo lilitokea katika Mji wa Kyaka mkoani Kagera wakati rais akielelekea Karagwe kwenye ziara yake. Ndani ya dakika tano baada ya kauli ya kukamatwa, Rais Magufuli aliagiza aachwe.

Akiwa kwenye ziara hiyo mkoani Kagera, Rais Magufuli alisimama kuzungumza na wananchi wa Mji wa Kyaka ambapo baada ya wafanyabiashara ndogondogo kulalamika kwamba, wanatozwa ushuru licha ya kukata vitambulisho vya ujasiriamali.

Malalamiko hayo yalimsukuma Rais Magufuli kumwita Mkurugenzi wa Wilaya ili kutoa majibu ya kwanini walio na vitambulisho wanatozwa ushuru.

“Mkurugenzi wa wilaya hapa uje hapa kwasababu watendaji wanaokusanya kodi wanatumwa na wewe… Je, uliwatuma wewe au walijituma wenyewe?” Rais Magufuli alihoji.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo alijitetea kwa kusema, hakuna aliyetumwa na ofisi yake kukusanya ushuru na kwamba, yeye kama mkurugenzi anatekeleza maagizo yake (rais).

“Sasa ni yupi anayekujaga kukusanya fedha hapa?” Rais Magufuli aliwahoji wananchi ambapo walimtaja Pesha. Rais alimwita Pesha kutoa maelezo na nani anayemtuma.

“Mheshimiwa Rais, sisi ofisini kwetu kuna utawala tofauti, mimi naagizwa na idara yangu ya mapato,” alisema Pesha na baada ya maelezo yake, Rais Magufuli alimwita Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo akisema “RPC mchukue huyu akalale lock-up akaeleze hizo fedha alizokusanya kwa watu wenye vitambulisho kazipeleka wapi.”

Baada ya hapo Rais Magufuli alimwagiza mkurugenzi kufuatilia fedha zilizokuwa zikikusanywa zilikuwa zikipelekwa wapi ama zikifanya nini.

“…Narudia tena…,kwa viongozi wote ndani ya serikali, mwenye kitambulisho hatakiwi kuombwa hela yoyote kwasababu wamelipia mwaka mzima,” alisema.

Kiongozi huyo wan chi aliwagiza wamachinga kutoweka biashara zao mbele ya madukwa ya walipakodi “huyu mwenye duka naye analipa kodi kubwa TRA, ninyi machinga msiende mkaziba biashara ya mtu.”

Pia alimwagiza mkurugenzi kufuatilia maofisa wake kwa kuwa, wanaweza kumuharibia kazi yake. Baada ya kauli hiyo alisema, “Pesha toka huko ndani, ngoja nimsamehe, mleteni hapa.

“… unajua naye ana watoto ila akirudia hiii! au twende naye tu? Tumsamehe? Mwachieni atubu kwa wananchi na wale waliotozwa muangalie namna ya kurudisha, mtoeni ila asirudie.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!