Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Mafuriko Bonde la Msimbazi: Kutoka hofu mpaka fursa
Makala & Uchambuzi

Mafuriko Bonde la Msimbazi: Kutoka hofu mpaka fursa

Spread the love

SASA ni wazi kwamba mafuriko yanayotokana na mvua kubwa zinazonyesha jijini Dar es Salaam tangu miaka ya 1990, yameikumbusha serikali ya Tanzania kuhusu umuhimu, uharaka na ulazima wa kubuni na kutekeleza jawabu la kudumu, dhidi ya mafuriko ya kila mara katika Bonde la Msimbazi. Anaandika Deusdedith Kahangwa, Dar es Salaam … (endelea)

Tayari serikali imekamilisha andiko linalofahamika kama “Mradi wa Msimbazi” kwa ajili hiyo.

Andiko hili limeandaliwa kwa kuzingatia ukweli kwamba, ndani ya Bonde la Mto Msimbazi, mvua zimekuwa zikisababisha mafuriko makubwa yenye kuhatarisha maisha ya raia, mali zao na miundombinu ya kiuchumi na kijamii kama vile barabara, madaraja, shule, hospitali na makazi ya watu.

Na sasa, huenda mateso haya kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, na hasa wale wanaokaa katika Bonde la Msimbazi, yakabaki ni historia. Tayari serikali ya Tanzania iko mbioni kutekeleza “Mradi wa Msimbazi” kwa ajili ya kukomesha maafa yanayotokana na mafuriko haya ya kila mwaka.

Kwa kushirikiana na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Uingereza (DFID), Benki ya Dunia (WB), na wadau wengine wa maendeleo, Serikali ya Tanzania imekamilisha andiko la “Mradi wa Msimbazi.”

Andiko hilo linataja mikakati ya kulifanya Bonde la Mto wa Mzimbazi kuwa mfano rejea wa suluhisho la kudumu dhidi ya majanga ya kibinadamu yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi, hasa katika maeneo ya mijini.

Kihistoria, mvua za El-Nino za mwaka 1997, ndizo zilianzisha mafuriko makubwa na hatarishi katika Bonde la Mto Msimbazi. Tangu wakati huo, yamekuwa yakitokea mafuriko karibu kila mwaka.  Mafuriko yaliyotokea katika mwaka 2009, 2010, 2011, 2014, 2015, 2017 na mwaka 2018. Na sasa, mwaka 2019 umeongezea matukio mengine ya mafuriko ya aina hiyo.

Kuandaliwa kwa andiko la “Mradi wa Msimbazi” ni matokeo ya juhudu za pamoja zilizofanywa kwa miezi 9 kati ya Januari na Agosti 2019, kupitia vikao 30, vilivyoshirikisha wawakilishi 150 kutoka taasisi 59, pamoja na wananchi wapatao 1000. Mchakato huu ulifadhiliwa na serikali ya Uingereza na kusimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Kwa ajili ya kuhuisha mchakato huu, hivi karibuni, ulifanyika mkutano maalum Jijini Dar es Salaam, tarehe 29 Novembea 2019. Katika mkutano huo, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, George Simbachawene, aliiwakilisha Serikali ya Tanzania.

Naye mwakilishi wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Uingereza (DFID) nchini Tanzania, Tim Bushell, aliwawakilisha wadau wa kimataifa waliofanya kazi kama wataalam washauri na wadhamini wa kifedha wakati wa kuandaa andiko la “Mradi wa Msimbazi.”

Dira ya “Mradi wa Msimbazi” ni kulibadilisha “Bonde la Msimbazi” kutoka katika hali ya kuwa bonde ambalo ni mzigo kwa wakazi wa Dar es Salaam, mpaka kuwa bonde ambalo ni mtaji kwao, kwa kufanikisha mabadiliko yafuatayo:

Kukomesha ujenzi holela unaolifanya Bonde la Msimbazi kupotosha mkondo wa maji ya mvua, kuhatarisha mifumo ya kiikolojia na kutishia maisha ya watu, kwa kuzalisha ujenzi uliopangiliwa kwa kuzingatia kanuni za mipango miji utakaoliwezesha Bonde la Msimbazi kuongoza vizuri mkondo wa maji ya mvua, kulinda mifumo ya kiikolojia na kuboresha maisha ya watu.

Dhima ya “Mradi wa Msimbazi” kwa ajili ya kufukuzia dira iliyotajwa hapo juu inataja maeneo makuu matatu ya kimkakati yanayogawanyika katika matawi makuu manne ya kiutekelezaji.

Katika eneo moja la kimkakati, dhima ya “Mradi wa Msimbazi” inaongelea kubadilisha “Bonde la Msimbazi” kutoka katika hali ya kuwa bonde ambalo ni adui wa mazingira, hadi kuwa bonde ambalo ni rafiki wa mazingira kwa kuchukua hatua tatu zitakazolifanya bonde hili liwe kama “mapafu katika mwili wa jiji.”

Katika eneo la pili la kimkakati, dhima ya “Mradi wa Msimbazi” inaongelea kubadilisha “Bonde la Msimbazi” kutoka katika hali ya kuwa bonde ambalo ni adui wa maisha ya watu, hadi kuwa bonde ambalo ni rafiki wa maisha ya watu kwa kuchukua hatua tatu zitakazolifanya liwe kama “moyo katika mwili wa jiji.”

Haya maeneo makuu manne ya kiutekelezaji (KRAs) yaliyo katika andiko la “Mradi wa Msimbazi” yamegawanywa katika mikakati 10.

Andiko la mradi huo linaonesha kuwa, jumla ya Dola za Marekani 114 milioni 1(Sh. 255 trililioni), zinahitajika ili kuukamilisha.

Godwin Cathbert Mapuga (52), kutoka Magomeni Mapipa, Mtaa wa Mwinyi Mkuu, Kata ya Mzimuni, ni mratibu wa Muungano wa Serikali za Mitaa 18 zilizo katika Bonde la Mto Msimbazi, kati ya Daraja la Salenda na Barabara ya Kawawa.

“Tukiwa ni wawakilishi wa wananchi tulijumuika pamoja na watu wengi wengi kama 200 katika vikao vya majadiliano yaliyoshirikisha wananchi ili kujua matatizo yetu. Vikao vile vilijulikana kama vikao vya Charrete. Tunatetea maslahi ya wakazi wa Bonde la Msimbazi,” alifafanua Mapuga.

Changamoto zilizomo katika bonde hiolo zinayo historia ndefu na hivyo, tayari zimeongelewa na vongozi mbalimbali wa ngazi za juu serikalini.

Selemani Jafo ni Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais kitengo cha TAMISEMI. Jafo ndiye waziri mwenye dhamana na mradi huu kwa niaba ya serikali.

“Sasa tunalo andiko la Mradi wa Msimbazi, na serikali ya Tanzania iko tayari kuutekeleza mradi huu, kwa kushirikiana na jumuiya ya wadau wa maendeleo,” anasema Jafo.

Kisha Waziri Jafo amesisitiza kwamba, ni muhimu na lazima kwa serikali kuunga mkono Mradi wa Msimbazi kwa sababu, kupitia mradi huu tunaweza kupata faida kuu mbili.

Nyariri Nanai ni mhandisi na mratibu wa mradi huo kupitia Ofisi ya Rais, Kitengo cha TAMISEMI. Tarehe 03 Januari 2020, mwandishi wa makala hii alimtembelea ili kujua utekelezaji wa “Mradi wa Msimbazi” umefikia hatua gani. Maongezi yalifanyika kwenye ofisi yake iliyoko katika Ofisi za TAMISEMI, ndani ya jengo la Millenium Tower, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.

“Sisi  TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, tunafanya upembuzi yakinifu ili kuona kama kukopa fedha kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Msimbazi ni mtaji au mzigo kwa Taifa, maana uamuzi wa kukopa fedha kutoka nje unamaanisha kuongezeka kwa deni la Taifa,” anafafanua Nanai.

Kwa mujibu wa andiko la mradi huo, sera ya ubia kati ya serikali na Sekta Binafsi (PPP) itatumika katika kuhakikisha fedha yote inayohitajika kwa ajili ya kukamilisha mradi huu inapatikana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

error: Content is protected !!