Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Kenyatta “Baba” wa demokrasia Afrika Mashariki
Makala & Uchambuzi

Kenyatta “Baba” wa demokrasia Afrika Mashariki

Uhuru Kinyata (kulia) na Raila Odinga
Spread the love

WAPINZANI nchini Kenya, wakiongozwa na Raila Odinga wa chama cha ODM na muungano wa NASA, wamekuwa wakipewa haki zote za kisiasa na za kidemokrasia bila kuminywa, anaandika Mwandishi Wetu.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amekuwa muungwana wa kipekee. Hata anapopewa nafasi ya kuzungumza katika ibada hususan kanisani na akamuona Odinga pia yupo eneo hilo, basi humkaribisha naye azungumze.

Wapinzani nchini Kenya walikuwa na madai mnalimbali katika kipindi cha uongozi wa miaka mitano ya Kenyatta na pia katika kipindi cha kukaribia uchaguzi mkuu kama ifuatavyo;

1. Kuna wakati waliomba kufanya maandamano yaliyoonekana kutokuwa na kikomo – waliruhusiwa, huku Mahakama nchini humu pia ‘ikiwalinda.’

2. Waliomba tume huru ya uchaguzi, ambayo bila shaka imefanya kazi kwa kasi na inatoa matokeo kwa kasi, ukiacha dosari ya kifo cha ofisa mmoja wa tume hiyo ambacho ukweli bado haujajulikana. Hata hivyo serikali imekuwa na unyenyekevu mkubwa ikiwemo kuomba radhi umma kwa kutomlinda ipasavyo ofisa huyo.

3. Ilikuwa ni madai ya wapinzani kuwa Wakenya waishio nje ya Kenya nao wapige kura -wakaruhusiwa.

4. Wakahitaji Uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara kila sehemu ya nchi – wakafanya bila kubughudhiwa.

5. Wakataka Uhuru wa vyombo vya habari bila kuvifungia, kuvitisha wala serikali kujigeuza wahariri wa vyombo hivyo – wakapewa.

6. Wakataka Uhuru wa kukosoa serikali yao kwa kadiri walivyotaka -hakusumbuliwa wala kushitakiwa kwa uchochezi.

7. Walitaka mpaka wafungwa wapige kura -wakaruhusiwa.

Kwa matokeo yanayoendelea kutokewa huku Kenyatta akiongoza kwa asilimia 55 dhidi ya 44 ya Odinga mpaka asubuhi ya leo, ni wazi Kenyatta atashinda miaka mitano mingine.

Hakika Kenyatta na Wakenya wanajua maana ya demokrasia, wanajua kuwa kamwe demokrasia na haki za kisiasa hazijawahi kuwa kikwazo cha uchumi wa viwanda wala maendeleo.

Uhuru Kenyatta amewafundisha “madikteta uchwara” wa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki na kati kuwa demokrasia ni kusikia hata yale usiyoyapenda, amewafundisha kuwa kuwashinda wapinzani si lazima uwapige mabomu, uwasweke rumande, uwanyanyase na uwanyime haki zao za kikatiba na kisheria.

Amewafunda kuwa nchi ni ya wote, si ya watawala peke yao. Hakika Kenyatta wewe ndiye Baba ya demokrasia katikati ya viongozi wa Kiimla wanaochipukia kwa kasi katika ukanda wetu. Hongera sana. Endelea kuiboresha Kenya na hakika viongozi wa nchi zingine wana mengi ya kujifunza kwako.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

error: Content is protected !!