Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini

Godbless Lema aitikia wito wa polisi

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameitikia wito wa Jeshi la Polisi uliomtaka kuwasili katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha bila kukosa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Lema amewasili katika ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, SACP Kamanda Ramadhan Ng’azi leo tarehe 22 Oktoba 2018.

Lema amewasili kituoni hapo kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano ambayo hadi sasa haijawekwa wazi kusudi la mahojiano hayo.

Taarifa za Lema kuitwa na Jeshi la Polisi alizitoa mwenyewe jana katika akaunti yake ya Twitter, akisema kuwa amepigiwa simu na polisi akitakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Arusha bila kukosa, bila ya kuelezwa sababu ya wito huo wa lazima.

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameitikia wito wa Jeshi la Polisi uliomtaka kuwasili katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha bila kukosa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). Lema amewasili katika ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, SACP Kamanda Ramadhan Ng’azi leo tarehe 22 Oktoba 2018. Lema amewasili kituoni hapo kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano ambayo hadi sasa haijawekwa wazi kusudi la mahojiano hayo. Taarifa za Lema kuitwa na Jeshi la Polisi alizitoa mwenyewe jana katika akaunti yake ya Twitter, akisema kuwa amepigiwa simu na polisi akitakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Arusha bila kukosa, bila ya kuelezwa sababu ya…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube