Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa January Makamba akamatwa, kisa kutekwa kwa MO
Habari za SiasaTangulizi

January Makamba akamatwa, kisa kutekwa kwa MO

Spread the love

JESHI la Polisi nchini, jana lilimhoji kwa saa kadhaa, January Makamba, kufuatia madai kuwa alikuwa chanzo kikuu cha taarifa za kutekwa kwa mfanyabiashara mashuhuri nchini, Mohammed Dewji (MO). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo zinasema, Makamba amekamatwa kwa tuhuma kuwa ndiye aliyekuwa kinara wa kutoa taarifa za kupotea, “kutekwa na aliko hifadhiwa MO.”

Kwa mujibu wa habari hizo, kilichomponza January ni mawasiliano yake na mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

Taarifa zinasema, Lema amekuwa akisambaza vijineno kuwa amekuwa na mawasiliano ya karibu na January na kwamba sehemu ya maelezo yake kwa waandishi wa habari juu ya mahali aliko MO, chanzo chake ni January.

“Anaweza kuwa ameponzwa na Lema. Huyu bwana mara kadhaa amekuwa akiripotiwa kumtaja January kama chanzo chake cha taarifa za kutekwa kwa MO,” ameeleza mmoja wa watu waliokaribu na Lema na January.

Anasema, “hata Lema ameitwa polisi. Inawezekana anatakiwa kuhojiwa kwa jambo hilohilo.”

Lema aliwahi kusema bungeni mazungumzo yake ya faragha kati yake na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, Charles Kitwanga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!