Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa DC apokelewa kwa mabango, awatupa rumande
Habari za SiasaTangulizi

DC apokelewa kwa mabango, awatupa rumande

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Kongwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Deo Ndejembi jana alijikuka katika wakati mgumu, baada wananchi wa kata ya Kikuyu Kaskazini kumpokea na mango yanye malaamiko mbalimbali yanayohusiana na mgoro wa ardhi. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Kutokana na hali hiyo Ndejembi alilazimika kuwaamuru askari wa jeshi la polisi kuwasweka baadhi ya wananchi rumande kutokana na kile kilichoonekana kuwepo kwa fujo  kutokubaliana katika maamuzi wakati wa mkutano wa adhara uliofanyika katani hapo.

Wakati akiingia katika mkutano wa hadhara ambao uliitishwa na Ndejembi kwa lengo ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi alikutana na mabango mbalimbali ambayo yalikuwa yameandikwa maneno kuwa, wanataka kupatiwa viwanja vyao ambavyo vinaonekana kuzulumiwa na uongozi wa kata kwa kushirikianana baadhi ya matajiri kujenga katika viwanja vya bila kulipwa hata fidia.

Katika mkutano huo wananchi walimtaka Ndejembi  kuingilia kati mgogoro wa mashamba ambayo unaonekana kuwa kero kubwa kwa wananchi waliokosa mashamba yao huku bila kujua hatima yao nan i lini watapimiwa na kumilikishwa.

Baadhi ya wananchi walisema kuwa wamekuwana mashamba yao kwa kuda mrefu lakini wameshindwa kujua ni lini watapatiwa haki yao kutokana na mashamba yao kuingiliwa na baadhi ya watu ambao ni wageni lakini wamekuwawakijenga katika mashamba yao.

Hata hivyo wananchi kwa nyakati tofauti walitumia jazba katika kumuuliza maswali mkuu huyo wa wilaya huku wakionesha kuwepo kwa malumbano jambo ambalo lilimpelekea Ndejembi kutoa amri kwa jeshi la polisi kuwakamata wananchi hao na kuwaeleka runande.

Hata hivyo Ndejembi alisema kuwa pamoja na mambo mengine yeye hakujua kama kuna tatizo kubwa la ardhi kama waliyoeleza wananchi na kudai kuwa atalifanyia kazi jambo hilo ili wananchi waweze kupata haki yao.

“Mimi sikujua kama kuna tatizo kubwa kiasi hicho lakini hata kama kuna matatizo jamani hatuwezi kuendesha nchi kwa mabango au kwa kutumia lugha za kuhudhi, mimi nimekuja hapa kusikiliza kero zenu lakini cha kushangaza ni kuona mnakuja namabango na nilisha taka nigeuze gari nirudi.

“Najua kabisa kuwa watu mnauchungu wa mali zenu lakini ni lazima tuheshimiane mimi ni mkuu wa Wilaya na nimwakilishi wa Rais hapa nilipo je anaweza kuja rais hapa mkamfanyia haya mliyoyafaya, mimi nafanya kazi kwa misingi ya ukweli na uwazi pamoja na utawala bora,” alisema Ndejembi.

Katika kutatua mgogoo huo Ndejembi alitangaza kusitisha ujenzi na kufanya shughuli yoyote ya kibinadamu hadi hapo atakapokuwa amejiridhisha kwa kupata takwimu sahihi za watu wenye maeneo na ni kwanini wamecheleweshwa kupimiwa na kupewa haki zao.

Hata hivyo ndejembi alisema Jiji kwa kitengo cha mipango miji wamekuwa wasababishaji wa migogoo kutokana na kutokuwa wepesi katika kutatua migogoro ya ardhi kwa wakati.

Aidha alisema Uongozi wa Jiji la Dodoma, wahakikishe wanatatua migogoro hiyo ikiwa ni pamoja na kupima maeneo haraka na kutoa majibu kwa wakati kwa wananchi wa maeneo husika badala ya kuwa na mrorongo mkubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!