
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani alipolazwa katika hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam
STEVEN Ngonyani aliyefahamika zaidi kwa jina la Profesa Majimarefu, Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), amefariki dunia leo usiku Jumatatu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Eligaeshi amethibitisha kutokea kwa kifo cha mbunge huyo aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo.
Prof. Majimarefu alianza kuugua akiwa bungeni jijini Dodoma tangu mwezi uliopita kabla ya kuhamishiwa Muhimbili Juni 20, mwaka huu. Ugonjwa uliokuwa ukimsumbua mbunge huyo hakikuwekwa wazi.
More Stories
Simba yaichapa Jkt, Yaisogelea Yanga
Dk. Mwinyi atoa fursa kwa wanahabari Z’bar
Rais Mwinyi ateua mrithi wa Maalim Seif