Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema wagoma mpaka 2020
Habari za SiasaTangulizi

Chadema wagoma mpaka 2020

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

KAMATI Kuu ya Chadema imeazimia kususia chaguzi ndogo zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni kutokana na kutoridhishwa na uendeshwaji wa chaguzi ndogo zilizopita. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Akizungumza kuhusu maazimio ya kamati hiyo iliyoketi jana tarehe 18 Septemba 2018 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amedai kuwa kumekuwa na hujuma katika chaguzi ndogo ikiwemo wakurugenzi kutumika katika kuhakikisha wagombea wa CCM wanapita bila kupingwa.

Mbowe amesema kamati hiyo imefikia uamuzi wa kutoshiriki chaguzi ndogo hasa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kwenye jimbo la Liwale na kata 37, baada ya  kutafakari yaliyotokea kwenye chaguzi ndogo za ubunge za Ukonga, Monduli na kata 23 Jumapili iliyopita ya Septemba 16, 2018.

“Kwa sasa tunakwenda kufanya mabadiliko ndani ya chama, tunakwenda kujijenga na hatuwezi kushiriki wakati tunaonewa na sheria hazifuatwi. Kwa sasa tunarudi nyuma,” amesema.

Mbowe ametaja baadhi ya matukio aliyodai kwamba yamebaka demokrasia, pamoja na wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wakurugenzi kufunga milango pindi wagombea wa Chadema wanaporudisha fomu pamoja na wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kutotambulika mapema huku suala hilo likifanyika kwa makusudi maalumu.

Matukio mengine aliyotaja Mbowe ni baadhi ya viongozi wa umma kufanya kampeni kinyume na sheria na baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi katika vituo vya wapiga kura ambapo mawakala walizuiliwa kuingia kutumika kupiga kura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!