Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polepole ajikanyaga Uchaguzi Ukonga
Habari za SiasaTangulizi

Polepole ajikanyaga Uchaguzi Ukonga

Spread the love

HUMPHREY Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amedai kwamba, mahudhurio hafifu ya wapiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ukonga umetokana na watu kwenda kazini. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Uchaguzi huo ulifanyika siku ya Jumapili ya tarehe 16 Septemba 2018, siku ambayo mara zote imekuwa ikitumika kwa kuwa, wananchi wengi hupata fursa ya kushiriki uchaguzi kutokana na kuwa kwenye mapumziko ya mwisho wa wiki.

Chaguzi zote (kuu na ndogondogo) hufanyika Jumapili kwa kuwa, wananchi kupata fursa ya kushiriki wakiwa kwenye mapumziko ya wiki.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 18 Septemba 2018 jijini Dar es Salaam Polepole amedai kuwa, mwitikio mdogo wa wapiga kura katika uchaguzi huo ni hali ya kawaida kutokana na historia ya chaguzi ndogo mbalimbali zinazofanyika Tanzania na duniani kote.

“Mi ninachokifahamu wapiga kura walikuwa laki tatu Ukonga, na waliopiga kura ni pungufu sana, na msingi wake ni mmoja tu, huu unaitwa uchaguzi mdogo.

“… na kwa historia hapa Tanzania na duniani kote na kwenye elimu ya michakato ya katiba, uchaguzi mdogo huwa una mwitikio mdogo sana, kwa sababu ni kipindi kati ya uchaguzi mkuu na uchaguzi mkuu. Pia watu wanakuwa kazini kutafuta maendeleo,” amesema Polepole.

Kwenye uchaguzi huo, waliopiga kura walikuwa ni asilimia 29.4 kati ya watu 300,609 waliotarajiwa kupiga kura ambapo mgombea wa CCM (Mwita Waitara) alitangazwa kushindwa kwa asilimia 89.1.

Amesema, CCM itaendelea kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili inapofika kipindi cha uchaguzi wajitokeze kwa wingi.

ambapo waliopiga kura walikuwa ni asilimia 29.4 kati ya watu 300,609 waliotarajiwa kupiga kura katika uchaguzi huo uliompa ushindi wa asilimia 89.1 mgombea wa CCM, Mwita Waitara.

Matokeo ya uchaguzi huo yamelalamikiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwamba, yamegubikwa na udanganyifu.

Ni pamoja na baadhi ya mawakala wao (Chadema) kucheleweshwa kuingia katika vituo vya kupigia kura kutokana na kuzuiliwa na wasimamizi wa uchaguzi.

Hata hivyo, yapo malalamiko ya idadi ya wapiga kura iliyotolewa kuwa kubwa tofauti na walioshiriki upigaji kura jambo ambalo halijatolewa ufafanuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!