April 11, 2021

Uhuru hauna Mipaka

167 wakutwa na Corona Kenya, wagonjwa wafikia 2,767

Mutahi Kagwe, Waziri wa Afya Kenya 

Spread the love

UGONJWA unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) nchini Kenya, umeendelea kushika kasi, baada  ya wagonjwa wapya 167 kupimwa na kukutwa na corona. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Kenya imekuwa na utaratibu wa kutoa taarifa ya corona kila siku ambapo jana Jumapili tarehe 7 Juni 2020, Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe alisema, ndani ya saa 24 zilizopita, walipima sampuli 2,833 na 167 kukutwa na maambukizo.

Kagwe alisema, kati ya hao 167, wanaume ni 125 na wanawake ni 42.

Waziri huyo alisema, wamewaruhusu wagonjwa 46 baada ya kupona corona hivyo kufikisha idadi ya waliopona corona kufikia 752,

Alisema, mgonjwa mmoja alifariki na kufikisha watu 84 waliofikiwa na mauti kwa ugonjwa huo.

Alisema, mpaka jana Jumapili, walikuwa wamepima sampuli 97,340 nchi nzima.

Jumamosi iliyopita tarehe 6 Juni 2020, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alihutubia taifa na kutoa maelekezo mbalimbali ikiwamo kuwataka Wakenya kuendelea kuchukua tahadhari kwani ugonjwa huo bado upo.

Alisema baadhi ya maeneo kama Nairobi, idadi ya wagonjwa wamekuwa wakiongezeka siku hadi.

Kutokana na hali hiyo, Rais Kenyatta alitangaza kuzifungua kwa awamu shule na vyuo kuanzia tarehe 1 Septemba 2020 huku zuio la usafiri wa anga likiendelea.

Alisema, anatamani kufungua shule, vyuo na shughuli zingine ziendelee kama kawaida lakini wataalamu wake, walimshauri kufanya hivyo ni kuwaua Wakenya.

“Mimi mwenyewe nilikuwa na nia ya kufungua…lakini ni mtu mjinga ambaye asikilizi kutoka kwa wataalamu wetu. Wametuambia kufungua ni makosa na kuhatarisha maisha ya Wakenya,” alisema Rais Kenyatta

error: Content is protected !!