Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Zuma akataliwa kugombea urais
Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love

TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa zamani Jacob Zuma kwenye kiny’anganyiro cha uchaguzi uliopangwa Mei mwaka huu na hivyo kuzua mvutano katika maandalizi ya uchaguzi huo. Inaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Sababu zilizotolewa na IEC juu ya kuzuiwa kwa Zuma ni kwamba inatokana na rekodi ya uhalifu ya kiongozi huyo iliyosababisha kupewa kifungo kinachozidi miezi 15. Zuma alikuwa anatarajiwa kushiriki uchaguzi kupitia chama kipya cha uMkhonto we Sizwe.

Nchi hiyo itafanya uchaguzi mkuu tarehe 29 Mei, uchaguzi ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi tangu ujio wa demokrasia mwaka 1994.

Chama tawala cha African National Congress (ANC) kiko katika hatari ya kupata chini ya asilimia 50 ya kura kwa mara ya kwanza tangu kilipoingia madarakani mwishoni mwa enzi ya utawala wa ubaguzi.

Chama kinazidi kupoteza wafuasi kutokana na uchumi dhaifu na madai ya ufisadi na usimamizi mbaya.

Zuma, mwenye umri wa miaka 81, alilazimika kuondoka madarakani mwaka wa 2018 chini ya wingu la madai ya ufisadi lakini bado ana umaarufu wa kisiasa.

Amekuwa akipiga kampeni kwa niaba ya chama cha upinzani cha uMkonto we Sizwe (MK) katika jaribio la kufufua tena hadhi yake, akiwaita wanachama wa chama chake cha zamani cha ANC, “wasaliti”.

“Kuhusu kesi ya rais wa zamani Zuma, ni kweli, tulipokea pingamizi, ambayo imekubaliwa,” mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Mosotho Moepya aliwaambia waandishi wa habari, bila kutoa maelezo zaidi.

Anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo kabla ya tarehe 2 Aprili 2024.

Katika hatua nyingine, jana, msafara wa Zuma ulipata ajali muda mfupi kabla ya saa 1:00 usiku wakati gari moja katika msafara wake lilipoanguka kati ya Gingindlovu na Eshowe huko KwaZulu-Natal.

Shirika la habari la News24 limethibitisha kuwa rais huyo wa zamani wala walinzi wake hawakupata majeraha yoyote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

error: Content is protected !!