Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Zuma akataliwa kugombea urais
KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Jacob Zuma
Spread the love

 

TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa zamani Jacob Zuma kwenye kiny’anganyiro cha uchaguzi uliopangwa Mei mwaka huu na hivyo kuzua mvutano katika maandalizi ya uchaguzi huo. Inaripoti Mitandao ya Kimtaifa … (endelea).

Sababu zilizotolewa na IEC juu ya kuzuiwa kwa Zuma ni kwamba inatokana na rekodi ya uhalifu ya kiongozi huyo iliyosababisha kupewa kifungo kinachozidi miezi 15. Zuma alikuwa anatarajiwa kushiriki uchaguzi kupitia chama kipya cha uMkhonto we Sizwe.

Nchi hiyo itafanya uchaguzi mkuu tarehe 29 Mei, uchaguzi ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi tangu ujio wa demokrasia mwaka 1994.

Chama tawala cha African National Congress(ANC) kiko katika hatari ya kupata chini ya asilimia 50 ya kura kwa mara ya kwanza tangu kilipoingia madarakani mwishoni mwa enzi ya utawala wa ubaguzi.

Chama kinazidi kupoteza wafuasi kutokana na uchumi dhaifu na madai ya ufisadi na usimamizi mbaya.
Zuma, mwenye umri wa miaka 81, alilazimika kuondoka madarakani mwaka wa 2018 chini ya wingu la madai ya ufisadi lakini bado ana umaarufu wa kisiasa.

Amekuwa akipiga kampeni kwa niaba ya chama cha upinzani cha uMkonto we Sizwe (MK) katika jaribio la kufufua tena hadhi yake, akiwaita wanachama wa chama chake cha zamani cha ANC, “wasaliti”.

“Kuhusu kesi ya rais wa zamani Zuma, ni kweli, tulipokea pingamizi, ambayo imekubaliwa,” mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Mosotho Moepya aliwaambia waandishi wa habari, bila kutoa maelezo zaidi.

Anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo kabla ya tarehe 2 Aprili.

Katika hatua nyingine, jana, msafara wa Zuma ulipata ajali muda mfupi kabla ya saa 1:00 usiku wakati gari moja katika msafara wake lilipoanguka kati ya Gingindlovu na Eshowe huko KwaZulu-Natal.

Shirika la habari la News24 limethibitisha kuwa rais huyo wa zamani wala walinzi wake hawakupata majeraha yoyote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!