Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto aukacha Urais, ataka kurudi bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Zitto aukacha Urais, ataka kurudi bungeni

Zitto Kabwe kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo
Spread the love

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo anayemaliza muda wake, Zitto Kabwe amesema hatogombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chake kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025, bali atagombea ubunge wa Kigoma Mjini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mwanasiasa huyo ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Februari 2024, akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Azam, baada ya kuulizwa kama atagombea urais au ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.

Zitto amesema kwa vyovyote vile anataka kurejea bungeni ili auimarishe mhimili huo akidai Bunge limerudi nyuma tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Wanachama wakinichagua kwamba niendelee (kumpitisha kuwa mgombea ubunge) nitagombea ubunge kwa sababu mimi kwa vyovyote vile nataka nirudi bungeni kwa sababu naamini kwamba miaka hii mitano ambayo hatukuwa bungeni Bunge limerudi nyuma,” amesema Zitto na kuongeza:

“ kuna matatizo kadhaa huwezi kulilaumu Bunge kwa ujumla wake lakini tunafahamu ni Bunge ambalo limetokana na mchakato wa uchaguzi ambao haukuwa wa kidemokrasia. Kwa hiyo tungependa kulirejesha Bunge lile kabla ya 2015 ili tuweze kutengeneza mazingira bora zaidi.”

Zitto amewahi kuwa mbunge wa Kigoma  katika vipindi tofauti ambapo 2005 alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo, hadi 2020 aliposhindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!