Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto augua ghafla Marekani
Habari za Siasa

Zitto augua ghafla Marekani

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalando
Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, ameugua ghafla akiwa nchini Marekani. Anaripoti Martin Kamotei, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya ugonjwa wa Zitto, imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Februari 2020, wakati kesi yake ya uchochezi namba 237/2018 inayomkabili, ikiendelea.

Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, leo alitarajiwa kutoa uamuzi kwamba Zitto ana kesi ya kujibu ama la, ni baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wake.

Ray Kimbita, mdhamini wa Zitto ndiye aliyeieleza mahakama kwamba, aliwasiliana na Nassor Mazrui, Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango wa ACT-Wazalendo ambaye yupo na Zitto nchini Marekani, ndipo alipoelezwa kiongozi huyo alishindwa kurejea kutokana na kuugua ghafla na amelazwa kwenye Hospitali ya Leesburg, Marekani.

“Alikuwa ameshakata tiketi kwa ajili ya kurejea nchini, ili ahudhurie kwenye kesi. Kutokana na kuugua kwake, madaktari wamempumzisha kwa siku 10,” amedai Kimbita.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga “kitendo cha mdhamini huyo kupigiwa simu na mtu mwingine, ina maana hajawasiliana na mshtakiwa na hajui alipo, atakaporudi aieleze mahakama sababu za kutowasiliana na mdhamini wake pamoja na udhibitisho wa kuugua.”

Wakili wa utetezi Steven Mwakibolwa, ameiomba mahakama kumpa muda ili mshtakiwa huyo aje kueleza kwanini hakuwasiliana na mdhamini pamoja na kuwasilisha nyaraka zitakazoonesha alikuwa mgojwa.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 18 Machi 2020 kwaajili ya uamuzi, pia amemtaka Zitto kufika mahakamani tarehe hiyo.

Tayari mashahidi 14 wa upande wa mashtaka, wametoa ushahidi katika kesi hiyo akiwemo Mkuu wa Upelelezi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, SSP John Malulu.

Kwenye mahakama hiyo, Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi. Anadaiwa kutenda makosa hayo tarehe 28 Oktoba 2018, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya Chama cha ACT – Wazalendo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Wazanzibar watarajia makubwa kutoka NMB Pesa Akaunti

Spread the loveWateja wapya wa Benki ya NMB wa Zanzibar wanatarajia neema...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kinana aungana na Tale kugawa mitungi ya gesi 800

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda amjibu Mwenyekiti UWT, “wananipa nguvu ya kuwapiga spana”

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukia Mwenyekiti wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madeni ya bilioni 219 yalipwa, wadai wengine waitwa

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia Mei mwaka 2021 hadi sasa imelipa madai...

error: Content is protected !!